Jan 24, 2022 07:57 UTC
  • Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani azidi kuitishia Russia

Huku akitumia maneno makali Antony Blinken Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ametoa vitisho kwa Russia na kuitahadharisha kuwa Moscow itakabiliwa na jibu kali la Marekani iwapo mwanajeshi mmoja tu wa Russia ataingia kiuhasama huko Uikraine.

Akiendelea kutoa vitisho dhidi ya Russia katika mahojiano aliyofanya na televisheni ya CNN, Blinken amesema eti Marekani imetetea kutokuwa na nia serikali ya Joe Biden kuiwekea Russia vikwazo vya awali licha ya Rais Volodymyr Zelinsky wa Ukraine kuiomba Marekani na waitifaki wake kuiadhibu Russia kwa hatua yake ya kutuma wanajeshi karibu na mipaka ya nchi hiyo.

Amesema lengo la vikwazo ni kuzuia hujuma ya Russia; na kwamba kama vitaanza kutekelezwa sasa dhidi ya Russia bila shaka vitapoteza taathira zake.  

Uhusiano wa Marekani na Magharibi na Russia umegubikwa na mivutano tokea mwaka 2014 pale kisiwa cha Crimea kilipoamua kujiunga na Russia.

Kisiwa cha Crimea kilichojiunga na Russia 

Eneo la Donbas linalokaliwa na raia wa Russia liko mashariki mwa Ukraine, na Russia iliasisi jamhuri mbili za Donetsk na Luhansk katika eneo hilo sambamba na kuunda serikali za majimbo zinazojiendeshea mambo yake zenyewe pasina na kuitegemea serikali ya Ukraine. 

Viongozi wa Russia mara kadhaa wametoa wito wa kufanyika mazungumzo kati ya serikali ya Ukraine na wawakilishi wa maeneo hayo mawili kwa lengo la kufikia muafaka na kuzipatia ufumbuzi hitilafu zilizopo lakini Kiev inaituhumu Moscow kuwa inauwanga mkono na kuwachochea wanaotaka kujitenga na hivyo imepinga kufanya mazungumzo na wawakilishi wa maeneo hayo mawili.  

Tags