Takriban watu 900 walisilimu pambizoni mwa Kombe la Dunia, Qatar
(last modified Sun, 27 Nov 2022 07:51:33 GMT )
Nov 27, 2022 07:51 UTC
  • Takriban watu 900 walisilimu pambizoni mwa Kombe la Dunia, Qatar

Hadi sasa watu 887 kutoka nchi tofauti wamesilimu kando ya Kombe la Dunia la mwaka huu wa 2022.

Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imeripoti kuwa, Zakir Naik, mwanazuoni wa Kiislamu wa India aliyekwenda Qatar kufanya tablighi na kueneza mafundisho ya Uislamu, amesema kuwa hadi sasa raia 887 kutoka nchi mbalimbali duniani wamesilimu pambizoni mwa mashindano Soka ya Kombe la Dunia.  

Naik ameongeza kuwa, usikiaji wa kisomo cha adhana huko Qatar umewaawathiri watazamaji wengi waliokwenda kushuhudia mashindano hayo ya soka ya dunia huko Qatar.  

Kombe la Dunia la Soka nchini Qatar 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Qatar pia inatekeleza ratiba mbalimbali za kuitangaza dini Tukufu ya Uislamu wakati huu sambamba na kufanyika mashindano hayo ya soka ya dunia.  

Mashindano ya Soka ya Dunia yanayoendelea sasa huko Qatar ni  Kombe la Dunia la 22 ambayo yameanza tangu Jumapili ya tarehe 21 mwezi huu wa Novemba; na yataendelea hadi tarehe 18 mwezi Disemba. Kombe la Dunia la Soka ndilo tukio la michezo linalotazamwa zaidi duniani na hufanyika kila baada ya miaka minne ili kumpata bingwa wa soka duniani.