Jan 16, 2023 03:09 UTC
  • Indhari ya UN: Sehemu kadhaa za dunia zitashindwa kukaliwa na watu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu taathira za mabadiliko ya tabianchi kuwa, athari za ongezeko la joto duniani zitakuwa haribifu; ambapo maeneo kadhaa ya dunia yatashindwa kukaliwa na watu.

Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha katika ujumbe alioutuma katika Mkutano wa 13 wa Taasisi za Kimataifa kuhusu nishati jadidika huko Abu Dhabi kuwa: jhadi kufikia karne ya 21 joto la dunia litafika daraja 2.8; ambapo athari za ongezeko hilo la joto zitakuwa mbaya.

Amesema aidha maeneo kadhaa ya dunia yatakuwa si mahali salama pa kuishi binadamu. Antonio Guterres aidha ameeleza kuwa, ni nishati jadidika pekee tu ndio itakayoweza kupunguza pengo katika kupatikana nishati, kuzifanya bei za nishati kuwa thabiti, kuhakikisha usalama wa nishati na kulinda mustakabali wa dunia.  

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa UN 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, vyanzo vya nishati jadidika kwa sasa vinachangia takribani asilimia 30 ya uzalishaji wa umeme duniani; ambapo  ili kuzalisha umeme nishati hiyo inapasa kuongeza kwa zaidi ya asilimia 60 hadi kufikia mwaka 2030 na kufikia asilimia 90 hadi katikati ya karne.   

Wawakilishi wa Umoja wa Mataifa  kuhusu mabadiliko ya tabianchi mwaka uliopita walitahadharisha kuwa ongezeko la joto duniani limeshindwa kudhibitiwa na binadamu ndio wanaopaswa kulaumiwa na kuwajibika kwa suala hilo.

Tags