Mar 18, 2023 14:17 UTC
  • Donald Trump
    Donald Trump

Rais wa zamani wa Marekani amesema kuwa Russia si tishio kubwa kwa Marekani bali baadhi ya raia wa nchi hiyo ndio tishio kwa Marekani na utamaduni wa Magharibi.

Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani amekosoa taasisi ya Wahafidhina Mamboleo na waungaji mkono wa utandawazi huko Marekani na kueleza kuwa, baadhi ya watu wanaoichukia Marekani ndio tishio kubwa zaidi kwa ustaarabu wa Magharibi leo hii. 

Trump ameongeza kuwa: Russia si tishio kuu dhidi ya utamaduni wa Magharibi, bali pengine zaidi ya chochote kile, sisi wenyewe na baadhi ya watu hatari wanaotuwakilisha na wenye chuki na Marekani ndio tishio kuu kwa nchi yetu."  

Wakati huo huo Donald Trump amewakosoa wale wanaounga mkono mfumo wa Kimaksi na kuwataja kuwa ni tishio kwa Marekani. Ameongeza kuwa, wafuasi wa utandawazi wanataka kupoteza nguvu, mali na damu ya watu wa Marekani. 

Trump amesema kuwa Ulaya ina wasiwasi mkubwa kuhusu Ukraine na kwamba vita vinavyoendelea katika nchi hiyo si suala la msingi linaloitia wasiwasi Marekani na ndio maana Ulaya inapasa kulipa gharama kubwa kutokana na vita hivyo.

Rais huyo wa zamani wa Marekani ameitahadharisha pia serikali ya Biden kwa kumwaga pesa na silaha huko Ukraine na hivyo kuiweka dunia katika ukingo wa maafa ya nyuklia.

Rais Joe Biden wa Marekani 

 

Tags