Mgombea urais wa Marekani: Robo ya Wamarekani wanalala na njaa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i96570-mgombea_urais_wa_marekani_robo_ya_wamarekani_wanalala_na_njaa
Robert F. Kennedy Jr anayewania kuwa mgombea rais wa Marekani amesema hali ya kiuchumi na kijamii katika nchi hiyo ni mbaya.
(last modified 2026-04-29T03:42:39+00:00 )
Apr 23, 2023 02:34 UTC
  • Mgombea urais wa Marekani: Robo ya Wamarekani wanalala na njaa

Robert F. Kennedy Jr anayewania kuwa mgombea rais wa Marekani amesema hali ya kiuchumi na kijamii katika nchi hiyo ni mbaya.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Mehr, Kennedy, ambaye alianza kampeni zake za uchaguzi siku mbili zilizopita, ametangaza katika taarifa kwamba robo ya watu nchini Marekani hawawezi kukidhi mahitaji yao na hulala na njaa.
Kulingana na mrithi huyo wa familia maarufu ya Kennedy, wanajeshi 33,000 wa zamani wa Marekani hawana makazi na hivi sasa ni miongoni mwa watu wasio na pa kuishi nchini humo.
Mwaniaji huyo wa nafasi ya kugombea urais wa Marekani ameendelea kwa kukumbusha kuhusu hali mbaya ya wanajeshi wa nchi hiyo na kueleza kwamba wanajeshi 23 wa Marekani hujiua kila siku.
Robert F. Kennedy Jr, mwenye umri wa miaka 69, mwanaharakati wa kisiasa ambaye anajulikana zaidi kwa kampeni yake ya kuzitoa thamani chanjo za corona, ametangaza nia ya kugombea uteuzi wa kuwania urais wa Marekani katika uchaguzi wa 2024 kwa tiketi ya Chama cha Democratic.
Yeye ni mpwa wa hayati John F. Kennedy, rais wa 35 wa Marekani.../