Marekani; tishio kubwa zaidi kwa usalama wa dunia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i99570-marekani_tishio_kubwa_zaidi_kwa_usalama_wa_dunia
Richard Haas, mwandishi na mchambuzi mashuhuri wa Marekani ametoa matamshi tata na kueleza kwamba, Marekani imebadilika na kuwa, chanzo kikuu cha ukosefu wa utulivu duniani na nchi hii ndiyo tishio kubwa zaidi kwa usalama wa dunia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 05, 2023 22:48 UTC
  • Marekani; tishio kubwa zaidi kwa usalama wa dunia

Richard Haas, mwandishi na mchambuzi mashuhuri wa Marekani ametoa matamshi tata na kueleza kwamba, Marekani imebadilika na kuwa, chanzo kikuu cha ukosefu wa utulivu duniani na nchi hii ndiyo tishio kubwa zaidi kwa usalama wa dunia.

Haas amefikia natija hiyo baada ya kuweko kwa miongo miwili katika asasi binafsi na mashuhuri zaidi ya Marekani katika uga wa Mahusiano ya Kigeni yaani Baraza la Mahusiano ya Kigeni.

Akizungumza katika mahojiano aliyofanyiwa katika siku yake ya mwisho kama mkuu wa Baraza la Mahusiano ya Kigeni, Haas alisema "Hali yetu ya kisiasa ya ndani sio tu kwamba, ni hali ambayo wengine hawataki kuifanya kuwa kiigizo, bali mimi nadhani inaonyesha kiwango cha kutotabirika na kutoaminiwa, jambo ambalo kwa hakika ni haribifu mno. 

Haas alionya kabla ya hapo, baada ya shambulio dhidi ya Congress ya Marekani Januari 6, 2021, juu ya kuporomoka Marekani katika medani ya ulimwengu kutokana na matukio ya ndani.

Kulingana na Haas, badala ya Marekani kuwa "nguzo ya kutegemewa zaidi katika ulimwengu uliotawaliwa na hali mbaya zaidi ya kutoaminiana, imegeuka na kuwa "chanzo kikuu cha ukosefu wa utulivu na mfano usiotegemewa wa demokrasia."

 

Richard Haas anaamini kwamba, kama kumeanza enzi ya baada ya Marekani, basi ni ileile siku ambayo, wafuasi wa Trump walivamia Bunge la Congress. Haas alionyesha wasiwasi wake juu ya matokeo ya tukio la kushambuliwa Kongresi katika sura ya kimataifa na kubainisha kwamba, ni jambo lililo mbali ulimwenguni kuweko mtu ambaye atatuangalia kama ilivyokuwa huko nyuma, akatuheshimu na kutuogopa. Ikiwa enzi ya baada ya Marekani ina mwanzo, basi hapana shaka siku hiyo ni leo. Kukiri mkuu wa kituo muhimu cha fikra cha sera za kigeni, kwa hakiika ni kuungama kupororomoka siku baada ya siku nchi hiyo katika medani na nyuga mbalimbali.

Wakati huo huo, tukitupia jicho utendaji wa Marekani katika kipindi cha baada ya vita baridi tunaona kuwa, Washington imekuwa na nafasi na mchango mkubwa katika kuzusha vurugu, machafuko na ukosefu wa usalama duniani. Baada ya tukio la Septemba 11, George W. Bush Rais wa wakati huo wa Marekani akitumia kisingizio cha kupambana na ugaidi ilitanguliza mbele utendaji wa uvamizi na akachukua hatua ya kuishambulia kijeshi Afghanistan na Iraq. Kufuatia sera hizo, zaidi ya watu milioni moja waliuawa katika mataifa ya Iraq, Afghanistan, Syria, Libya na Yemen. Kukaliwa kwa mabavu Iraq kulipekea kuibuka makundi ya kigaidi kama Daesh ambalo lilifanya jinai nyingi na za kutisha katika nchi za Iraq na Syria.

Pamoja na hayo, utumaji majeshi ya Marekani katika mataifa hayo haukuwa na natija yoyote kwa Washington. Hatimaye Marekani ikalazimika kuondoa askari wake huko Afghanistan baada ya kushindwa na kufeli vibaya. Pamoja na hayo, hadi sasa Marekanii ingalii ina askari katika nchi za Iraq na Syria.

Vita hivyo eti vya kupambanana ugaidi mbali na kusababisha maelfu ya askari wa Marekani kuuawa na kujeruhiwa vimeitwisha mzigo mkubwa bajeti ya nchi hiyo ambapo kwa mujibu wa Donald Trump Rais aliyepita wa Marekani, gharama hizo zinafikia dola trilioni saba. Ukweli wa mambo ni kuwa, aliyefadika na hujuma na hatua hiyo ya kijeshi ya Marekani baada ya shambulio la Septemba 11 ni mashirika ya utengenezaji na uzalishaji silaha ya Marekani.

Pamoja na hayo yote, serikali ya sasa ya Rais Joe Biden imeamua kufuata mkondo wa utendaji wa kichangamoto mkabala na madola makubwa ya kimataifa ambayo ni washindani wa Washington yaani China na Russia.

Shambulio la kigaidi la Septemba 11

 

Katika uga huo sambamba na kushadidisha mizozo katika eneo la Asia ya Pasific dhidi ya Chiina, Marekani iimeendelea kuitumia silaha na zana za kijeshi Ukraine na hivyo kuandaa uwanja wa kuendelea vita vya Russia na Ukraine.

Viongozi wa Russia wametangaza mara chungu nzima kuhusu nafasi haribifu ya madola ya magharibi yakiongozwa na Marekani katika kuandaa uwanja na mazingira ya lazima ya kutokea vita vya Ukraine. Ukweli wa mambo ni kuwa, vita vya Ukraine vinaweza kutathminiwa kuwa ni natija ya dhana mbaya na muamala ya kihujuma wa madola ya Magharibi hususan Marekani dhidi ya Russia.

Katika radiamali ya hatua za chuki na uadui za Marekani, mataifa ya Russia na China yakiwa madola mawili makubwa na muhimu kimataifa, katika miaka ya hivi karibuni yamechukua hatua muhimu kwa ajili ya kupanua ushirikiano na vilevile kuwa na misimamo mimoja dhidi ya siasa na hatua za upande mmoja za Marekani na yanataka kuweko utendaji wa pande kadhaa kama msingi wa nidhamu mpya ya kimataifa.

Moscow na Beijing zinaamini kwamba, matukio ya kimataifa yanathibitisha ukweli wa nidhamu ya kimataifa ambaye inapiga hatua kuelekea nidhamu ya kambi kadhaa. Hii ni katika hali ambayo, ikifanya juhudi za kujionyesha kuwa ni kiongozi wa dunia Marekani imekuwa ikifuatilia malengo na matakwa yake binafsi kupitia utendaji na uchukuaji maamuzi ya upande mmoja.