Jumatatu, 17 Februari, 2025
(last modified Mon, 17 Feb 2025 02:33:29 GMT )
Feb 17, 2025 02:33 UTC
  • Jumatatu, 17 Februari, 2025

Leo ni Jumatatu 18 Shaaban 1446 Hijria sawa na 17 Februari 2025.

Siku kama ya leo miaka 1125 iliyopita, sawa na tarehe 18 Sha’ban mwaka 321 Hijiria, alifariki dunia Ibn Dorayd, mtaalamu wa lugha, mwanafasihi na malenga wa Kiarabu.

Ibn Dorayd alikuwa mtaalamu, mwenye tabia njema na mkarimu. Alisifika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kumbukumbu.

Miongoni mwa vitabu vyake mashuhuri ni pamoja na kile alichokipa jina la "Al-Ishtiqaq" ambacho kimeandikwa kwa mpangilio wa herufi za Kiarabu. Vilevile ameandika diwani na tungo za mashairi.   

Siku kama ya leo, miaka 1120 iliyopita, sawa na tarehe 18 Sha’ban mwaka 326 Hijiria, alifariki dunia Abul-Qasim Hussein bin Ruh Naubakhti, naibu wa tatu wa Imam wa Zama, al Mahdi (as).

Abul-Qasim Hussein Naubakhti alikuwa, mtaalamu aliyetabahari katika elimu ya Hadithi, fiqihi na teolojia. Alipata umashuhuri mkubwa baina ya Waislamu mjini Baghdad, Iraq katika zama za uhai wake. Mwanazuoni huyo alifahamika pia kwa jina la Aal Naubakhti. Mwaka 305 na 326 Hujiria, Naubakhti, alikuwa naibu na mwakilishi wa Imam Mahdi (as) na wasita baina ya mtukufu huyo Waislamu. Imam Mahdi (as) alighibu, baada ya watawala wa enzi hizo kutaka kumshika na kumuua, alienda ghaiba kwa amri ya Allah SW. Imam wa Zama atadhihiri tena Akheri Zamani kwa amri ya Mwenyezi Mungu. 

kabuuri la bul-Qasim Hussein bin Ruh Naubakhti

Siku kama ya leo miaka 216 iliyopita, vilimalizika vita vya umwagaji damu vya Zaragoza vilivyopiganwa kati ya wanajeshi wa Ufaransa na wale wa Uhispania. 

Ufaransa ilipata ushindi katika vita hivyo na kuukalia kwa mabavu mji wa Zaragoza ulioko mashariki mwa Uhispania. Vita hivyo vilianza Novemba 15 mwaka 1808, kufuatia uvamizi wa jeshi la Napoleon.  

Katika siku kama ya leo miaka 198 iliyopita, aliaga dunia Johann Heinrich Pestalozzi, msomi wa Uswisi na mmoja wa walimu mashuhuri.

Pestalozzi alikuwa mjuzi wa elimu nyingi hasa hisabati na tiba na alizungumza lugha kadhaa za kimataifa.

Msomi huyo wa Uswisi alikuwa na mtindo wake makhsusi wa kufundishia ambapo aliweza kutoa mafunzo ya masuala mbalimbali kwa watoto kwa wakati mmoja. 

Johann Heinrich Pestalozzi

Katika siku kama ya leo miaka 36 iliyopita, mkataba wa kuasisiwa Jumuiya ya Magharibi ya Kiarabu za ulitiwa sana huko Morocco kwa kuhudhuriwa na Marais wa nchi za kaskazini mwa Afrika.

Nchi washiriki wa mkataba huo zilikuwa Libya, Mauritania, Algeria, Tunisia na mwenyeji Morocco. Lengo la kuasisiwa jumuiya hiyo lilikuwa kuanzisha taasisi ya kieneo kwa lengo la kupanua ushirikiano baina ya nchi wanachama na kupunguza utegemezi kwa nchi za Magharibi.

Hata hivyo, hitilafu za kimitazamo za baadhi ya wanachama wa Jumuiya ya Magharibi ya Kiarabu kama Algeria na Morocco kuhusiana na suala la Sahara Magharibi na vilevile mizozo ya mipaka na kisiasa zilizuia kufikiwa malengo ya kuasisiwa jumuiya hiyo. 

Tarehe 17 Februari miaka 14 iliyopita ilianza harakati ya wananchi wa Libya dhidi ya utawala wa kidikteta wa Kanali Mummar Gadafi.

Libya ilikuwa nchi ya tatu kukumbwa na wimbi la mwamko wa Kiislamu na kuziangusha tawala kadhaa za kidikteta. Baada ya kuondolewa madarakani serikali ya Zainul Abidin bin Ali nchini Tunisia na ile wa dikteta wa zamani wa Misri, Husni Mubarak, wananchi wa Libya pia walianzisha harakati kubwa dhidi ya dikteta wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi.

Awali Gaddafi alidhani kwamba angeweza kuzima harakati hiyo ya wananchi kwa kutumia jeshi na vyombo vya usalama na kwa msingi huo alianza kutumia mkono wa chuma na kuua wananchi waliokuwa wakiandamana. Wanachama wa shirika la kijeshi la nchi za Magharibi NATO pia walipanda mawimbi ya harakati ya mapinduzi ya wananchi wa Libya na kushambulia vituo vya kijeshi na viwanda vya Libya.

Hatimaye dikteta Muammar Gaddafi aliyeitawala Libya kwa kipindi cha miongoni minne kwa mkono wa chuma aliondolewa madarakani kwa madhila na kuuawa kwa kudhalilishwa na kisha akazikwa sehemu isiyojulikana. 

Mummar Gadafi

Siku siku kama ya leo miaka 8 iliyopita Mohamed Hassanein Heikal mwandishi na mwanafikra mtajika wa Misri alifariki dunia.

Mohamed Heikal alizaliwa Septemba 23 1923 katika jimbo la Qalyubia huko Misri. Alikuwa mhariri mkuu katika gazeti la al-Ahram la Misri kwa muda wa miaka 17. Heikal alikuwa muasisi wa kituo mashuhuri cha utafiti wa kisiasa na kiistratejia cha al-Ahram. 

Mohamed Hassanein Heikal