May 25, 2024 02:07 UTC
  • Jumamosi, 25 Mei, 2024

Leo ni Jumamosi tarehe 16 Mfunguo Pili Dhul-Qaadah 1445 Hijria mwafaka na 25 Mei 2024 Miladia.

Siku kama ya leo, miaka 664 iliyopita, yaani tarehe 25 Mei mwaka 1360 kundi la mabaharia wa Kifraransa liligundua Ghuba ya Guinea. Ghuba ya Guinea iko magharaibi mwa bara la Afrika katika bahari ya Atlantiki. Baada ya muda kupita tangu kugunduliwa Ghuba ya Guinea, ushawishi wa Ufaransa ndani ya bara hilo ulianza, na taratibu ikaanza kuidhibiti ardhi iliyokuja kujulikana baadaye kama Guinea. Nchi ya Guinea iliendesha harakati za mapambano ya miaka mingi mpaka ikafanikiwa kupata uhuru wake mwaka 1958. Guinea ina eneo lenye ukubwa wa kilomitamraba zaidi 245,000 na imepakana na nchi za Senegal, Guinea Bissau, Mali, Ivory Coast, Liberia na Sierra Leone. ***

Siku kama ya leo miaka 136 iliyopita Ayatullah Zainul Abidin Mazandarani mmoja wa maulamaa wakubwa wa Kiirani aliaga dunia. Baada ya kuhitimu masomo ya awali, Ayatullah Mazandarani alielekea katika hauza ya kielimu ya Najaf huko Iraq ili kukamilisha masomo ya kidini. Akiwa huko mwanazuoni huyo alifunzwa na maustadhi wakubwa wa zama hizo wa hauza ya Najaf kama vile Sheikh Murtadha Ansari na kufikia daraja ya juu ya kielimu na kimaanawi. ***

Katika siku kama ya leo miaka 116 iliyopita, kisima cha kwanza cha mafuta cha Iran kilianza kuchimbwa huko katika mji wa Masjid Suleiman kusini magharibi mwa Iran. Mafuta ya kisima hicho yalifikiwa umbali wa kina cha mita 600, mafuta ambayo hatimaye yaliruka hadi kufikia urefu wa mita 25 kutoka uso wa ardhi. Mji wa Masjid Suleiman una umuhimu mkubwa kutokana na upatikanaji wa madini na vyanzo vya mafuta. Ni vyema kutaja hapa kuwa Iran ni moja ya nchi muhimu duniani kwa kuwa na akiba kubwa ya mafuta na ni nchi ya pili yenye akiba kubwa ya gesi duniani baada ya Russia. ***

Miaka 61 iliyopita katika siku kama ya leo, yaani tarehe 25 Mei mwaka 1963, Hati ya Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) ilisainiwa mjini Addis Ababa, Ethiopia kwa kuhudhuriwa na viongozi wa nchi 32 za bara hilo. Marais Gamal Abdel Nasser wa Misri, Kwame Nkrumah wa Ghana na Ahmed Sekou Toure wa Guinea walikuwa miongoni mwa waasisi wa jumuiya hiyo. Jumuiya ya OAU ilielekeza jitihada zake katika kuleta umoja kati ya nchi za Afrika, kutatua hitilafu kati ya nchi hizo, kutetea haki ya kujitawala ya nchi wanachama na ukombozi wa nchi nyingine za Kiafrika zilizokuwa zingali zinakoloniwa. Mnamo mwezi Julai mwaka 2002, viongozi wa nchi wanachama wa OAU walifanya kikao nchini Afrika Kusini na kuamua kubadilisha jina la jumuiya hiyo kutoka Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) na kuwa Umoja wa Afrika (AU) sambamba na kuanzisha taasisi kadhaa kwa ajili ya utekelezaji wa maamuzi ya umoja huo na kustawisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi wanachama. Hivi sasa Umoja wa Afrika una nchi 54 wanachama. Makao Makuu ya umoja huo yako Addis Ababa, Ethiopia na kikao cha viongozi wa nchi wanachama hufanyika kila mwaka katika moja ya nchi hizo. ***

Miaka 19 iliyopita katika siku kama hii ya leo aliaga dunia Ustadh Rahim Moazzen Zadeh Ardabili mwadhini mashuhuri wa Kiirani. Alizaliwa katika familia ambayo ilikuwa ikishughulisha zaidi na harakati za kidini na kuuadhini. Rahim Moazzen Zadeh Ardabili alikuwa mtoto mkubwa wa Sheikh Abdul-Karim na alifuata njia ya baba yake kwa nguvu zake zote.  Baada ya kufariki dunia baba yake, Rahim Moazzen Zadeh Ardabili akaendeleza kazi ya mzazi wake huyo ya kuadhini. Hatimaye mwadhini huyo mashuhuri wa Iran aliaga dunia katika siku kama ya leo akiwa na umri wa miaka 80. ***

Katika siku kama ya leo miaka 116 iliyopita, kisima cha kwanza cha mafuta cha Iran kilianza kuchimbwa huko katika mji wa Masjid Suleiman kusini magharibi mwa Iran. Mafuta ya kisima hicho yalifikiwa umbali wa kina cha mita 600, mafuta ambayo hatimaye yaliruka hadi kufikia urefu wa mita 25 kutoka uso wa ardhi. Mji wa Masjid Suleiman una umuhimu mkubwa kutokana na upatikanaji wa madini na vyanzo vya mafuta. Ni vyema kutaja hapa kuwa Iran ni moja ya nchi muhimu duniani kwa kuwa na akiba kubwa ya mafuta na ni nchi ya pili yenye akiba kubwa ya gesi duniani baada ya Russia. ***