Jumapili, 9 Juni, 2024
Leo ni Jumapili tarehe Pili Mfunguo Tatu Dhul-Hijja 1445 Hijria sawa na tarehe 9 Juni mwaka 2024 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 1956 iliyopita katikak siku kama ya leo, Mfalme Nero Claudius Caesar mtawala katili na aliyemwaga damu nyingi wa Rome alijiua, baada ya kuishi kwa miaka 31 na kutawala kwa maiaka 14. Si vibaya kuashiria hapa kwamba Nero aliasiliwa na mjomba wake Mfalme Claudius aliyekuwa mtawala wa kwanza wa Rome. Lakini Nero alimpa sumu mfalme huyo na kuchukua nafasi yake baada ya kufa. Mfalme huyo katili na wa mwisho wa Rome, wakati wa utawala wake aliwaua watu wengi wa familia yake akiwemo mama yake, mkewe, kaka yake na ndugu zake wengine. Pia aliwaua wananchi wake wengi. Aliwaua kwa umati Wakiristo pamoja na kuuchoma moto mji wa Rome. ***
Miaka 139 iliyopita muwafaka na leo, jeshi la Ujerumani lilivamia ardhi ya Togo huko magharibi mwa Afrika. Wakati huo maeneo ya pwani ya Togo yalipendelewa zaidi na watu wa Ulaya kwa ajili ya biashara ya utumwa. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana Togo imekuwa maarufu kwa jina la "Pwani ya Utumwa." Wakoloni wa Ujerumani waliendelea kuikalia kwa mabavu ardhi ya Togo hadi wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. Baada ya hapo Togo ilikoloniwa na Wafaransa na Waingereza. Nchi hiyo ilipata uhuru mwaka 1960. ***
Siku kama ya leo miaka 62 iliyopita moto mkubwa ulitokea katika Chuo Kikuu cha Algiers mji mkuu wa Algeria. Moto huo ulichoma zaidi ya nakala laki tano za vitabu vyenye thamani kubwa zilizokuwa kwenye maktaba ya chuo hicho. Asilimia kubwa ya vitabu vilivyoungua vilikuwa miongoni mwa marejeo muhimu na nadra. Chuo Kikuu cha Algiers na maktaba yake vilichomwa moto na jeshi la siri la Ufaransa nchini Algeria. Jeshi hilo la siri liliundwa na askari wa Ufaransa waliokuwa wakipinga suala la kupewa uhuru Algeria. Moto huo ulikuwa miongoni mwa makumi ya mioto kadhaa iliyotokea katika siku hiyo nchini Algeria na mingi ilisababishwa na jeshi la siri la Ufaransa.
Siku kama ya leo miaka 54 iliyopita, aliuawa shahidi Ayatullah Sayyid Muhammad Reza Saeedi, mmoja wa wasomi wakubwa na wanamapambano wa Iran baada ya kuteswa kwa muda mrefu katika mojawapo ya jela za utawala wa kitwaghuti wa Shah. Alielekea mjini Qum na kujiunga na chuo cha kidini cha mji huo na kupata elimu kwa maulama wakubwa akiwemo Ayatullahil-Udhma Borujerdi na Imamu Khomein (MA). Baada ya mwamko wa mapinduzi ya wananchi Waislamu nchini Iran, tarehe 15 Khordad 1342 Hijiria, alidizisha harakati zake dhidi ya utawala wa kidikteta wa Shah. Katika uwanja huo, Ayatullah Sayyid Muhammad Reza Saeedi aliufanya msikiti wake kuwa ngome ya kuwazindua na kuwahamasisha wananchi hususan vijana, na hotuba zake nyingi zilijikita katika kufichua njama chafu za ukoloni na jinai za utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya watu madhlumu wa Palestina. Ni kwa sababu hiyo ndio maana alikamatwa mara kadhaa na kufungwa jela. Hata hivyo vitendo hivyo vya utawala wa Shah havikuweza kuathiri hata kidogo katika azma ya mwanazuoni huyo mtajika wa Kiislamu. Miongoni mwa athari za Ayatullah Sayyid Muhammad Reza Saeedi ni pamoja na kitabu cha ‘Umoja wa Kiislamu’ ‘Uhuru wa Mwanamke’ na ‘Kazi na Uislamu. ***
Katika siku kama ya leo miaka 43 iliyopita, Bani Sadr Rais wa kwanza wa Iran baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliuzuliwa na Imam Khomeini wadhifa wa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote kutokana na kusalitii nchi. Tangu awali baada ya kuchaguliwa kuwa Rais, Bani Sadr alikumbwa na kiburi na ghururi na akawa anafuatilia suala la kuwaweka kando wanamapinduzi watiifu kwa Imam Khomeini, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Bani Sadr pia alikuwa akishirikiana na makundi yaliyokuwa yakipinga Mapinduzi ya Kiislamu. Vilevile alikwamisha utendaji wa serikali kutokana na kukwepa kwake kumkubali Waziri Mkuu Muhammad Rajai mmoja wa wanamapambano mashuhuri aliyekuwa amechaguliwa na Bunge kwa wingi wa kura. Ukwamishaji huo wa Bani Sard ulifikia kileleni katika vita vya kichokozi vya Iraq dhidi ya Iran na kupelekea miji mingi ya Iran katika kipindi hicho cha vita kukaliwa kwa mabavu na utawala wa dikteta Saddam Hussein. Hatimaye katika siku kama ya leo, Imam Khomeini alimuuzulu Bani Sadr cheo cha Amiri Jeshi Mkuu. Siku chache baadaye Bunge lilipasisha kwa wingi wa kura kutokuwa na imani na uwezo wa kisiasa Rais huyo. ***