Jumanne, 11 Juni, 2024
Leo ni Jumanne 4 Mfunguo Tatu Dhul-Hija 1445 Hijria mwafaka na 11 Juni 2024 Miladia.
Katika siku kama ya leo miaka 452 iliyopita sawa na tarehe 11 Juni mwaka 1572, alizaliwa Benjamin Jonson (Ben Johnson) mshairi na mwandishi wa filamu wa Uingereza. Jonson kwa muda mrefu alikuwa mcheza tamthilia na rafiki wa Shakespare mwandishi maarufu wa Uingereza, ambapo urafiki wao ulikuwa na athari kubwa katika kukamilisha fasihi ya mshairi huyo. Baadhi ya athari zilizoachwa na Benjamin Jonson ni Mwanamke Aliyezimwa' pamoja na Historia ya Dunia. Malenga huyo Muingereza alifariki dunia mwaka 1637. ***
Siku kama ya leo miaka 169 iliyopita inayosadifiana na tarehe 11 Juni mwaka 1855, mwanga wa jua ulitambuliwa kwa kutumiwa njia za taaluma ya uchanganuzi na wigo wa rangi. Jaribio hilo lilifanywa kwa mara ya kwanza katika historia ya utafiti mpya wa fizikia na wanasayansi wawili wa Ujerumani walioitwa Kirchhoff na Bunsen. Si vibaya kuashiria hapa kwamba, mionzi ya jua katika hewa wakati wa mvua pamoja na kutokea upinde wa mvua wenye rangi mbalimbali, ni tukio la kuvutia ambalo linasababishwa na kuchanganuliwa nuru ya jua na matone ya maji mawinguni. Hata hivyo suala hilo mwanzoni lilifafanuliwa na wanasayansi wa Kiislamu kama vile Ibn Sina, Ibn Haitham na Qutbuddin Shirazi na baadaye kuthibitishwa na Kirchhoff na Bunsen. ***

Katika siku kama ya leo miaka 64 iliyopita, Muhammad Hussein Fadhil Toni, msomi na mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu aliaga dunia katika mji wa Tehran Iran. Alizaliwa 1257 Hijria Shamsia huko Ferdows kaskazini mashariki mwa Iran. Katika kipindi cha kutafuta elimu, Toni alihudhuria darsa na masomo ya waliimu mahiri wa zama zake. Fadhil Toni alikuwa mahiri zaidi katika elimu kama za Fiq'h, hisabati, nujibu, fasihi, erfan na kadhalika ***
Miaka 31 iliyopita katika siku kama ya leo, Rasul Montazeri mwanadiplomasia wa Kiislamu alikuwa akifanya kazi katika ubalozi wa Iran mjini Zagreb mji mkuu wa Croatia aliuawa shahidi na wanamgambo wa Croatia. Mwanadiplomasia huyo aliuawa shahidi wakati akitekeleza jukumu la kupeleka misaada ya Iran kwa Waislamu Bosnia Herzegovina waliokuwa wahanga wa vitendo na hatua za kibaguzi za Waserbia. ***