Ukoloni, tangu mwanzo hadi leo (8)
Assalaamu Alaykum wasikilizaji wapenzi. Podkasti ya "Ukoloni, tangu mwanzo hadi leo" mbali na kutoa maana ya fikra chafu ya ukoloni, inatoa pia historia na namna fikra hiyo ya kikatili ilivyosababisha maafa makubwa katika maeneo tofauti ya dunia. Podkasti hii inazungumzia mpya ukoloni katika aina zake mbalimbali.
Karibuni katika episodi hii ya 8 ya mfululizo wa Podkasti ya "Ukoloni tangu mwanzo hadi leo." Baada ya kutoa maelezo ya kutosha kuhusu vipindi tofauti ulivyopitia ukoloni katika episodi zilizopita, tulizungumzia makundi mbalimbali ambayo yalisaidia fikra ya kikoloni kufikia malengo yake machafu. Baada ya hapo tulichunguza mbinu mbalimbali zilizotumiwa na wakoloni katika upande wa kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kadhali. Episodi iliyopita imezungumzia suhula na zana zilizotumiwa na wakoloni ikiwa ni pamoja na propaganda za mashirika ya habari, redio za kimataifa, kanali za satalaiti, televisheni ya kimataifa, ulimwengu wa filamu, sinema na animation, majarida mitandao ya Intaneti, vitabu n.k.
Katika episodi hii ya nane tutazungumzia zana na suhula nyingine zinazotumika kuendeleza fikra ya kikoloni yaani zana ya elimu. Ni matumaini yangu mtakuwa nami hadi mwisho wa episodi hii ya 8 ya podikasti ya "Ukoloni, tangu mwanzo hadi leo."
****************
Wakoloni wanatumia mbinu na suhula zote za kudhibiti mfumo wa elimu na usomeshaji ili kila nukta ya sekta hiyo muhimu mno iweze kutumia malengo haramu ya kikoloni. Mfumo wa elimu, matini na vitabu vya kufundikisha, vituo vya elimu na walimu, lugha za nchi za Ulaya kama Kiingereza na Kifaransa na misingi ya kiutamaduni ni miongoni mwa zana za elimu na ufundishaji ambazo zinatumiwa moja kwa moja na wakoloni ili kufanikishia malengo yao machafu.
Mfumo wa Elimu:
Mfumo mpya wa elimu ambao umebuniwa na Ulimwengu wa Magharibi na unatumika takriban katika kona zote za dunia, muda wote una nafasi kubwa sana katika kuendeleza fikra za kikoloni duniani. Mfumo huo wa Elimu umebuniwa kwa mujibu wa mila na utamaduni wa madola ya Magharibi, fikra za kisekula na kumpinga Mungu zimejaa ndani yake na umehakikisha masuala ya kimaanawi na kiroho yanawekwa pembeni kikamilifu.
Mfumo mpya wa elimu uliobuniwa na madola ya Magharibi umesimama juu ya msingi ambao ambao hauendani kabisa na maumbile na maadili mema ya kibinadamu. Bali lengo lake kuu ni ni kufundisha maarifa na kuandaa nguvu kazi yenye utaalamu unaotakiwa na mashirika ya uzalishaji ya madola ya Magharibi. Wanaohitimu kwenye mfumo huo wa elimu wa nchi za Magharibi kwenye nchi mbalimbali duniani hasa za Waislamu, wamegawika kwenye mafungu matatu makuu:
1 - Ni fungu la watu wachache sana ambao wanathamini masuala yao ya kiitikadi na kiutamaduni na wanaendelea kushikamana na mila na desturi zake ambao hawana imani sana na mfumo huo mpya. Ni watu ambao wanaendelea kuheshimu matukufu yao ya kimaanawi na hawaathiriwi na tamaduni chafu za Magharibi.
2 - Kundi la pili ni la watu waliochanganyikiwa ambao hawajui washike wapi. Wako katikati hawako kwenye masuala ya kiroho kikamilifu lakini pia hawakutekwa kikamilifu na mila na desturi za madola ya Magharibi.
3 - Fungu la tatu na ambalo ndilo kubwa zaidi ni wale wanaoathiriwa vibaya na mila na desturi za Magharibi kutokana na mfumo huo mpya wa elimu. Watu hao wanapoteza kabisa imani za kiroho na matukufu yao na wanajikita tu kwenye kujidhisha mahitaji yao ya kimaada na kimwili. Kwa vile watu hao wanaziona nchi za kikoloni zimeendelea zaidi katika upande huo wa kimaada kuliko nchi zao, wanaamua kuzitegemea kwa kila kitu nchi hizo za kikaoloni na muda wote wanafanya mambo yao kuhakikisha hawawakasirishi mabwana zao hao.
Pembeni mwa Mfumo wa Elimu, matini na vita vya kufundishia ni silaha nyingine inayotumiwa vibaya na mabeberu na wakoloni dhidi ya mataifa ya dunia. Vitabu vya masomo ambavyo ndivyo vinavyodhamini malengo machafu yanayotumikia wakoloni, vinaandikwa kwa upendeleo maalumu na muda wote vinahakikisha vinamuelekeza mwanafunzi upande uliokusudiwa na madola ya kiistikbari na matokeo yake ni kujenga vizazi vya watu ambao wanaabudu Umagharibi na wanatumika kikamilifu kufanikisha malengo ya kikoloni.
Amma katika upande mwingine, vituo vya elimu na wahadhiri wa vyuo vikuu waliofunzwa katika mfumo wa elimu wa nchi za Magharibi na ambao ni waendelezaji wa mfumo huo wa elimu, ndani na nje ya nchi za Magharibi, ni chombo cha kuzalisha nguvukazi inayotakiwa na madola ya kibeberu, Yumkini vituo na wahadhiri hao wakaleta mabadiliko fulani katika mfumo wa kibeberu, lakini hilo si jambo la kutegemewa kutokea kila siku. Lakini wako wahadhiri ambao kwa kupenda nchi zao na mataifa yao, huwa wanafanya jitihada kubwa za kuleta ubunifu wa mifumo mipya ya kielimu ili kuziletea ustawi na maendeleo nchi zao.
Wenzo mwingine unaotumiwa ambao ni maaarufu hivi sasa ni kulazimisha matumizi ya lugha ya Kiingereza. Kuifanya lugha ya Kiingereza kuwa lugha ya kielimu na ya kimataifa ambapo hata maprofedha na wahadhiri wa kimataifa wanalazimishwa kuisoma na kuitambua vizuri, mbali na kupelekea kuenea sana matumizi ya lugha hiyo ya kikoloni, kunachochea pia kuenea utamaduni wa Magharibi katika nchi nyingine. Suala hilo linafuatiliwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenye tasnia ya filamu. Unapotupia jicho yaliyomo kwenye filamu ambazo zinatumika kufundishia lugha ya Kiingereza zinatumika pia kueneza mambo machafu na maadili yasiyo ya kibinadamu.
Suhula nyingine ni taasisi na vituo vya kiutamaduni. Vituo na taasisi za kiutamaduni zinaubeba sana mfumo wa kikoloni kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kazi zao za kutoa mafunzo ya vitu mbalimbali. Miongoni mwa taasisi hizo zinazotumika kuendeleza na kufanikisha malengo ya ukoloni ni Ford Foundation, Carnegie Foundation, USA Aid, Peace Corps na Rockefeller Foundation ni katika taasisi maarufu ambazo zinatumika kufanikisha malengo ya kikoloni. Kidhahiri na kijuujuu taasisi hizo zinaonekana ni za kutoa misaada ya kibinadamu kwa mataifa mengine duniani, lakini uhakika wa mambo ni kwamba ni nyenzo kuu za kufanikisha malengo ya kikoloni na kibeberu. Sababu yake ni kwamba, mashirika ya kibepari ambayo yanataka kubapa faida kubwa kutoka nje yanazitegemea sana taasisi kama hizo za kiutamaduni na kimisaada kwa ajili ya kueneza aidoiolojia zao na kuwalazimisha watu wa mataifa mengine kuwa waraibu wa kutumia bidhaa zinazozalishwa na mashirika hayo ya kibepari.
Katika karne ya 20, mashirika hayo ya Marekani yaliwekeza sana katika kuyafanya mazingira ya nchi zinazoendelea kuwa na sura nyingine kabisa ya kijamii kwa mujibu wa malengo yanayotakiwa na madola ya kikoloni na ili iwe rahisi kunyoywa utajiri wa nchi hizo na kuknufaisha mikakati ya kiuchumi ya Marekani. Wakuu na watungaji sera wa taasisi zinazoidhibiti Marekani walikuwa wanaelewa kikamilifu kwamba kama ambavyo mfumo wa kibeberu umejikita mno katika masuala ya kimaada, unaweza kufanikisha pia mambo yake kwa kutumia mbinu za kiitikadi na kiaidiolojia. Mabeberu wanatambua kuwa, shughuli za kila siku, mara nyingi zinatokana na fikra za watu katika masuala yao ya kila siku na jambo hilo linaweza kutumiwa kwa manufaa ya mabeberu kunufaisha nguvu za kisiasa na kiuchumi za madola ya kikoloni.
Taasisi kama hizo zina nafasi kubwa katika kusafisha sura ya madola ya kikoloni kwa mataifa mengine. Kwa kweli taasisi hizo zinatumika kupandikiza na kuendeleza utamaduni na itikadi za kikoloni kwa watu wa mataifa mengine kiasi kwamba haziruhusu watu kuelewa uhakika wa mambo na hata unapokuja kudhihirika ukweli wa mambo, mazingira yaliyoandaliwa na taasisi hizo hayaathiri sana katika misimamo na imani za watu wa mataifa hayo.
Kiujumla ni kwamba taasisi za kiutamaduni za madola ya Magharibi kwa nchi za Afrika, Asia na Amerika ya Latini zote zina lengo moja, nalo ni kuhakikisha nchi za Afrika, Asia na Amerika ya Latini zinakuwa tegemezi milele kwa mashirika ya kibepari ya kikoloni yakiwemo ya Marekani.
Tunaendelea kuchambua suhula na zana zinazotumiwa na ukoloni kwa ajili ya kuendeleza malengo yao haramu dhidi ya mataifa mengine duniani. Sasa ni wakati wa kuzitupia jicho taasisi za kimataifa na kuangalia ni jinsi gani zinatumika kufanikisha malengo haramu ya kiistiimari.
Taasisi za kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa IMF, Benki ya Dunia na Shirika la Biashara la Kimataifa zinajionesha kwa walimwengu kuwa ni mashirika ya kimataifa yanayopigania haki za wanadamu wa mataifa yote, lakini kimsingi ni nyenzo za kufanikisha malengo ya mabeberu.
Tukiangalia historia ya taasisi za kimataifa na kujitokeza kwake, tutaona kuwa zinagawika kwenye mafungu mawili makuu:
1 - Taasisi ambazo tangu mwanzo kabisa zimeanzishwa juu ya msingi wa kikoloni na kukandamiza mataifa mengine.
2 - Taasisi ambazo misingi ya kuanzishwa kwake haikuwa ya kikoloni. Ziliasisiwa na watu wenye nia njema na kwa malengo ya kutoa misaada ya kweli ya kibinadamu kwa ajili ya kuwatatulia watu matatizo yao na kusaidia wanaokumbwa na majanga mbalimbali. Lakini baada ya kupita muda malengo ya kuasisiwa mashirika na taasisi hizo yamebadilika na kutumiwa vibaya na wakoloni kwa ajili ya kufanikisha malengo yao ya kiistikbari.
Umoja wa Mataifa: Hiki ndicho chombo kikubwa zaidi cha kimataifa lakini katika historia yake yake yote hadi hivi sasa chombo hicho kimeshindwa kuchukua hatua yoyote ya maana ambayo inakwenda kinyume na matakwa ya madola ya kibeberu.
Mfuko wa Kimataifa wa Fedha na Benki ya Dunia ambayo iliasisiwa mwaka 1945 nayo pia kazi yake kubwa ni kutumikia malengo ya kikoloni. Sababu yake ni kwamba kila nchi iinayowekeza zaidi kwenye taasisi hizo na kila mwenye hisa kubwa zaidi ndiye mwenye sauti ya juu. Nchi za Magharibi zimewekeza sana kwenye taasisi hizo kwa ajili ya kudhibiti masuala ya kiuchumi ya dunia na ndio maana taasisi hizo mbili nazo zikawa hazifurukuti mbele ya amri na udikteta wa madola ya kibeberu na kiikoloni.
Shirika la Biaishara Duniani ambalo liliundwa mwaka 1995 hivi sasa linafuata mkondo ule ule wa kufanikisha malengo ya kkolonii ulimwenguni. Kwa mfano: Sharti la kujiunga na shirika hilo ni kutambua mkataba wa kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake suala ambalo halina uhusiano wowote na masuala ya uchumi na biashara. Kkwa kweli sharti hilo limewekwa ili kusaidia utekelezaji wa siasa za kikoloni za utamaduni na kupandikiza na kutia nguvu mila na desturi za madola ya Magharibi katika nchi nyingine ulimwenguni.
Shirika jingine la kimataifa ambalo linatumikia malengo haramu ya madola ya kibeberu duniani, ni Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA). Shirika hilo liliiundwa mwaka 1957 na lengo lake hasa ni kukzuia uzalishaji na uenezaji wa silaha za nyuklia na kuleta ushirikiano wa kimataifa wa kuhakiikisha tenkolojiia na nishati hiyo muhimu sana inatumika kwa malengo ya kiraia yasiyo na madhara kwa dunia. Lakini hivi sasa shirika hilo linaendesha mambo yake kwa manufaa ya madola ya kikoloni na kiistiimari.
Hati ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, Mkataba wa Kuondoa Ubaguzi dhidi ya Wanawake na Makubaliiano ya Kuzuia Kuenea Silaha za Atomiki yote hiyo ni mikataba na makubaliano ya kimataifa ambayo inatumika moja kwa moja kufanikisha malengo ya kikoloni na kiisikbari duniani. Kwa mfano, Hati ya Kimataifa ya Haki za Binadamu imeandaliwa kwa kuzingatia mtazamo wa kimaada wa Magharibi kuhusu mwanadamu. Hati hiyo ina mapungufu mengi sana, lakini hivi sasa imelazimishwa iwe ni hati ya kimataifa ambayo kila nchi duniani inalazimishwa kuifuata hata kama inapingana na matukufu yake. Lakini cha ajabu na cha kuchekesha zaidi ni kwamba, nchi zenyewe za Magharibi ndio viranja wa kutoheshimu vipengee vya haki hiyo lakini zinaitumia kukandamiza nchi nyingine ambazo hazikubaliani na siasa zao za kikoloni na kibeberu.
Mashirika na vyama vya siasa ambavyoi vinatumikia kwa siri malengo ya ukoloni maarufu kwa jina la Freemasonry pia vinatumika kufanya ujasusi, kukusanya na kuajiri mawakala wa ukoloni katika nchi nyingine. Pia, magenge ya kigaidi na kimafia kila moja linatumikia malengo ya kikoloni na kibeberu kwa upande wake. Kwa mfano, moja ya nyenzo muhimu zinazotumiwa na ukoloni kuimarisha udhibiti wake wa mataifa mengine duniani, kueneza matumizi ya mihadarati na madawa ya kulevya na kuwalemaza kiakili vijana wa mataifa mengine. Madawa hayo hatari na haramu yana athari kubwa mbaya katika kuwadhibiti watu wa mataifa yanayokoloniwa. Hivyo magenge ya mafia na ya kigaidi na kimafia yanasaidia moja kwa moja ufanikishaji wa malengo haramu ya kikoloni.
Mashirika ya kutoa huduma mbalimbali kama vile shirika la mikahawa la McDonald la Marekani, kijuujuu utaliona ni shirika la kutoa huduma za vyamakula tu lakini kumbe lengo lake kuu ni kupandikiza utamaduni wa Marekani na Magharibi katika mataifa mengine.
****************
Wasikilizaji wapenzi tunaendelea na podkasti hii kwa kujadili jinsi madola ya kikoloni yanayoendesha sera za kuyafanya mataifa mengine yayafanye kigezo madola hayo ya kiistikbari ikiwa ni muendelezo wa siasa za kikoloni za madola ya Magharibi.
****************
Sote tunajua kuwa wanadamu wanahitaji kuwa na vigezo vya watu wa kuigwa. Wakoloni wanatumia vibaya dhati hiyo ya wanadamu kuwaelekeza watu wa mataifa mengine kwenye vigezo chapwa na visivyofaa ili kufanikisha malengo yao ya kikoloni. Kwa bahati mbaya, watu wengi wanafanya makosa na hawako makini hata kidogo katika kuchagua vigezo vya kufuata. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema haya kuhusu vigezo umuhimu ambavyo vinapaswa kuzingatiwa katika kuchagua ruwaza na mtu wa kumfanya kuwa kigezo chako.
"Si kila anayetaka kigezo na kila anayetafuta ruwaza njema ya kufuata anapatia katika chaguo lake. Kuna watu dunia ambao ukiwauliza sura gani imeiteka akili yako? Utaona wamewafuata watu hakiri, wadogo, waovu na wasio na maadili mema hata kidogo ambao wamepitisha umri wao wote katika kuaburu hawaa na matamanio ya nafsi. Vipaji pekee vya watu hao ni mghafala unaowapumbaza kwa muda watu wasio na hadhi na waliokumbwa na mghafala kama hao. Watu wa namna hiyo ndio wanaofanywa kuwa vigezo na baadhi ya watu duniani."
Mambo ambayo wakoloni wanayalazimisha yafanywe vigezo na mataifa mengine ili waweze kuendeleza ukoloni wao ni pamoja na:
1. Wakoloni wanawatumia wanawake na wanaume wanaopachikwa majina makubwa kama vile wasanii, warembo, wasichana waliostaarabika na wanaokwenda na wakati ili kuharibu kizazi kipya na kukipotosha na kuwaongoza watu kwenye maisha ya duni ya kupenda mali na anasa chapwa za kughuririsha na za kupita za kidunia.
2. Wakoloni wanahamisha uvunjaji wa sheria, mila na desturi za mataifa mengine kwa kutumia majina tofauti kama vile "Rap," "Heavy Metal," "Playboy" na kadhalika
3. Wakoloni wanawachochea watu kuwafanya vigezo nyota wa michezo na wale ambao wamefanya michezo kuwa njia ya kujikuza na kupata umaarudu duniani lakini ukiwaangalia wanavunja mila na desturi nzuri za vijana wa mataifa mengine katika hali ambayo inaishia kufanya utamaduni wa Magharibi kuwa kigezo kikuu cha kufuata.
4. Watu wanaodai kuwa ni watu wa kiroho na kimaanawi lakini kumbe umaanawi wao ni kidhabi na wa uongo ambao wanautumia kuwapotosha watu kwa shabaha ileile ya kutumikia malengo ya kikoloni.
5. Wakuu wa vyama na wakuu wa makabila ya zamani ambao wanawalazimisha watu wawafuate kibubusa bila ya kutumia akili zao. Hawa nao wanatumikia malengo ya kikoloni kupitia kuwafanya watu wajinga na mbumbumbu wasio na uwezo wa kuamua.
6. Vibonzo, katuni, vinyago na wanasesere ambao wanatumika kuchezea hisia za watoto maskini na wasio na hatia na kuwaelekeza kwenye kutumikia malengo ya wakoloni. Mfano wazi wa michezo hiyo ya katuni ni kama "Barbie" ambayo imetengezwa Marekani na ni njia ya kuendeleza na kupandikiza utamaduni wa Marekani na wa kikoloni.
**********************************************
Wasikilizaji wapendwa mambo tuliyoyataja kwenye episodi hii ya nane ya podikasti ya Ukoloni tangu mwanzo hadi leo ni sehemu ndogo tu ya mbinu zinazotumiwa na wakoloni kufikia malengo yao haramu. Katika kipindi kijacho, tutajadili madhara na maafa ya ukoloni tukijaaliwa. Tunakatibisha maoni yenu kupitia WhatsApp na Telegram yetu ya +989035065487 na B-pepe yetu ya [email protected] kuhusu podikasti hii. Mtandao wetu wa Intaneti ni parstoday.ir/sw. Kama mna ushauri au kuna maudhui yoyote mnapenda tuiandikie podikasti, msisite kutujulisha.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.