Mar 01, 2025 02:57 UTC
  • Jumamosi, 01 Machi, 2025

Leo ni Jumamosi 30 Shaaban 1446 Hijria sawa na tarehe Mosi Machi 2025 Miladia.

Katika siku kama ya leo miaka 210 iliyopita, ufalme wa siku mia moja wa Napoléon Bonaparte ulianza nchini Ufaransa baada ya Bonaparte kutoroka sehemu aliyokuwa amebaidishwa katika kisiwa cha Elba. Tarehe 27 mwezi Februari mwaka huohuo akiwa pamoja na wanajeshi elfu moja Napoleon Bonaparte alifanikiwa kutoroka katika kisiwa cha Elba ambako alikaa akiwa uhamishoni kwa kipindi cha miezi kumi na kurejea Ufaransa na utawala wa kifalme ukaanza nchini humo. 

 

Miaka 154 iliyopita katika siku kama ya leo, kufuatia kuushindwa vibaya Ufaransa na Ujerumani, Bunge la Taifa la lilimuondoa mfalme katika cheo chake na kufuta mfumo wa kifalme katika nchi hiyo ya bara Ulaya. Kikao hicho cha Bunge kilikuwa kimeitishwa kwa ajili ya kutathmini mazingira yya mapatano na Ujerumani. Kwa uamuzi huo, mfumo wa kifalme ukawa umefutwa nchini Ufaransa ikiwa ni baada ya kupita miaka 82 tangu kutokea mapinduzi nchini humo. Baada ya apinduzi ya ufaransa ya 1789, kwa mara ya kwanza Napoleon Bonapart alikuwa amejitangaza kuwa mfalme na baada yyake shakhsia wengine walishikilia cheo hicho.

 

Siku kama ya leo miaka 133 iliyopita yaani tarehe 1 Machi mwaka 1892, alizaliwa mjini Tokyo mwandishi na mtaalamu mkubwa wa Japan anayejulikana kwa jina la Ryunosuke Akutagawa. Mwandishi huyo anahesabika kuwa mmoja wa waasisi wa kanuni mpya za fasihi huko Japan. Akutagawa ameacha athari muhimu ikiwa ni pamoja na vitabu vya "Binti wa Buibui" na "Tushi Gun."Mwandishi huyo alifariki dunia mwaka 1927. 

 

Miaka 127 iliyopita katika siku kama leo, kisiwa cha Puerto Rico kilichoko katika ya Bahari ya Atlantic kaskazini mwa Amerika ya Kusini, kilikaliwa kwa mabavu na vikosi vya majeshi ya Marekani baada ya kumalizika vita vya kikoloni vya Uhispania na Marekani. Baada ya Marekani kukitwaa kwa nguvu kisiwa hicho ilikifanya ghala kubwa la silaha, kiasi kwamba Marekani iliasisi kambi 13 za kijeshi kisiwani humo. Kisiwa hicho ambacho mara kwa mara hukumbwa na ukosefu wa amani, miongoni mwa nchi zinazozungumza lugha ya Kihispania katika bara la America. 

 

Katika siku kama ya leo miaka 50 iliyopita, Chama cha Rastakhiz kiliundwa nchini Iran kwa amri ya Muhammad Reza, mfalme wa mwisho wa ukoo wa Pahlavi. Kwa utaratibu huo Iran ikawa rasmi nchi ya chama kimoja na vyama vichache vilivyokuwa vikifanya harakati zake chini ya uangalizi wa utawala wa kifalme vikavunjwa. Chama cha Rastakhiz ulikuwa wenzo wa mfalme Shah kwa ajili ya kufikia malengo yake haramu hususan kuimarisha udikteta wake na kuwadhibiti zaidi wananchi kupitia uanachama wao katika chama hicho.