Aug 08, 2016 06:46 UTC
  • Jumatatu, tarehe 08 Agosti

Leo ni Jumatatu tarehe 5 Dhilqaada 1437 Hijria mwafaka na tarehe 8 Agosti mwaka 2016.

Siku kama ya leo miaka 2349 iliyopita, sawa na tarehe 8 Agosti 333 kabla ya kuzaliwa Nabii Issa Masih AS, ilianza kazi ya ujenzi wa mji wa Alexandria wa kaskazini mwa Misri, ambao leo hii unahesabiwa kuwa moja kati ya bandari muhimu kusini mwa Bahari ya Mediterranean. Ujenzi huo ulifanyika kwa amri ya Alexander The Great aliyejulikana pia kama Alexander of Macedon aliyekuwa katika kilele cha nguvu na madaraka wakati huo nchini Misri.

Na siku kama ya leo miaka 739 iliyopita Ghiathuddin Abu Mansur Abdul Karim bin Ahmad anayefahamika kwa lakabu ya Ibn Taus, faqihi na mwandishi mashuhuri wa karne ya saba Hijria alifariki dunia huko Kadhimein, moja kati ya miji ya Iraq. Ibn Taus alihifadhi Qur'an Tukufu akiwa na miaka 11. Alipata umashuhuri mkubwa baina ya wanazioni wa zama hizo kutokana na takwa, uchamungu na elimu yake kubwa. Umashuhuri mkubwa zaidi wa mwanazuoni huo wa hadithi, historia na fasihi unatokana na kunukuu haditi zinazohusiana na amsuala ya kimaadini na teolojia ya Kiislamu. Miongoni ma vitabu muhimu vya msomi huyo mkubwa nui Al Luhuuf fi Qatlat ufuuf kinachozungumzia historia ya mauaji ya mjukuu wa Mtume Muhammad Imam Hussein (as) katika siku ya Ashuraa na kile cha al Malahimu Wal Fitan kinachohadithia matukio ya kabla na wakati wa kudhihiri Imam wa Zama, Mahdi (as).

Miaka 18 iliyopita katika siku kama ya leo inayosadifiana na tarehe 8 Agosti 1998, wanamgambo wa kundi la Taliban nchini Afghanistan waliuteka na kuukalia kwa mabavu mji wa Mazar Sharif ulioko kaskazini mwa nchi hiyo. Baada ya kukaliwa kwa mabavu mji huo, wanamgambo wa Taliban waliushambulia ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mji huo na kuwauwa shahidi wanadiplomasia 8 wa Kiirani na mwandishi mmoja wa habari. Kundi la Taliban liliasisiwa mwaka 1994 kwa ufadhili na usaidizi wa Marekani na Pakistan na kufanikiwa kuikalia sehemu kubwa ya ardhi ya Afghanistan.  

 

 

Tags