Aug 13, 2016 08:18 UTC
  • Kianoush Rostami, Bingwa wa mchezo wa kunyanyua uzani wa Iran
    Kianoush Rostami, Bingwa wa mchezo wa kunyanyua uzani wa Iran

Bingwa wa mchezo wa kunyanyua uzani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelishindia taifa hili medali ya kwanza ya dhahabu sambamba na kuvunja rekodi ya dunia katika mashindano ya Olimpiki ya Rio yanayoendelea nchini Brazil.

Kianoush Rostami mwenye uzito wa kilo 85, ameshinda medali ya dhahabu katika mchezo wa kunyayua vyuma vizito baada ya kunyanyua uzani wa kilo 396.

Medali ya fedha imemuendea Mchina Tian Tao aliyenyanyua uzani wa kilo 395 huku raia wa Romania Gabriel Sincraian akifunga orodha ya tatu bora kwa kushinda medali ya shaba.

Muirani Kianoush Rostami huko Rio nchini Brazil

Mara baada ya kushinda medali hiyo siku ya Ijumaa na kuvunja rekodi ya dunia kwa kilo moja zaidi, Rostami aliwaambia waandishi wa habari kuwa: "Makocha wa Kiirani ni wazuri na wenye tajriba ya hali ya juu, lakini hakuna mtu aliyejua kuwa mimi nimefika kiwango hiki bila ya mkufunzi. Nimekuwa nikifanya mazoezi binafsi kisiri. Majaaliwa tutakutana katika Olimpiki ya Tokyo mwaka 2020 na natumai kung'ara zaidi."

Wanamichezo wengine wanaotazamiwa kuiweka Iran ya Kiislamu katika ramani ya dunia huko Rio de Janairo ni Sohrab Moradi katika mchezo wa kunyanyua uzani kitengo cha kilo 94 na Behdad Salimikordabiasi katika safu ya uzani mzito almaarufu super-heavyweights.

Tags