Aug 15, 2017 02:29 UTC
  • Jumanne 15 Agosti, 2017

Leo ni Jumanne tarehe 22 Dhulqaada 1438 Hijria sawa na Agosti 15, 2017.

Siku kama ya leo miaka 902 iliyopita inayosadifiana na tarehe 21 Dhulqaad mwaka 536, kazi ya uandishi wa tafsiri maarufu na kamili ya Qur'ani Tukufu inayojulikana kwa jina la Majmaul-Bayaan ilikamilika. Kitabu hicho kiliandikwa na Sheikh Tabarsi mmoja katu ya wafasiri wakubwa wa Qur'ani wa Iran ambaye kutokana na umashuhuri na uaminifu wake katika elimu za fikihi, hadithi na tafsiri ya Qur'ani alijulikana kkwa lakabu ya Aminul Islam, jina linalomaanisha kuwa mtunza amana wa Uislamu. Tafsiri ya Majmaul Bayaan ni miongoni mwa tafisri muhimu sana za Qur'ani na imechapishwa mara kadhaa katika nchi mbalimbali kama Iran, Misri na Lebanon.

Tafsiri ya Qur'ani ya Majmaul Bayaan

Tarehe 24 Mordad miaka 81 iliyopita alifariki dunia alimu na mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu Mirza Muhammad Hussein Naini. Alizaliwa katika eneo la Nain nchini Iran na baada ya kupata elimu ya msingi alielekea katika mji mtakatifu wa Najaf huko Iraq kwa ajili ya kupata elimu ya juu. Ayatullah Naini alipata nafasi maalumu kati ya maulamaa wa Najaf kutokana na elimu na maarifa yake ya kina katika elimu za hesabati, falsafa, irfan na fiqhi. Alikuwa hodari sana katika elimu ya usulul fiqhi. Allamah Naini ameandika vitabu vingi kama kile cha "Tanbihul Umma" kinachohujumu tawala za kidikteta. Vitabu vingine vya mwanazuoni huyo ni Wasilatun Najat na Taqrirat.

Mirza Muhammad Hussein Naini

Miaka 57 iliyopita katika siku kama ya leo mwafaka na tarehe 15 mwezi Agosti mwaka 1960 Jamhuri ya Kongo maarufu kwa jina la Kongo Brazaville ilipata uhuru. Kongo ilikuwa sehemu ya ardhi ya Kongo iliyozijumuisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Zaire ya zamani) na Angola. Kongo Brazaville iligunduliwa na Wareno katika karne ya 15 na baadaye ilikaliwa kwa mabavu kwa miaka kadhaa na wakoloni wa Kifaransa.

Miaka 27 iliyopita katika siku kama ya leo, inayosadifiana na tarehe 24 Mordad 1369 Hijria Shamsia, Saddam Hussein Rais wa zamani wa Iraq alimtumia barua Hujjatul Islam Walmuslimin Hashemi Rafsanjani aliyekuwa Rais wa Iran kwa wakati huo, akimjulisha kwamba amekubali kikamilifu vipengee vya makubaliano ya mpaka yaliyotiwa saini 1975 nchini Algeria. Hata hivyo, tarehe 27 Shahrivar 1359 Hijria Shamsia, Saddam Hussein baada ya kushawishiwa na madola ya kibeberu ya Magharibi, alijitokeza kwenye televisheni ya Iraq na kuuchanachana mkataba huo, na baada ya siku chache, aliivamia ardhi ya Iran. Saddam Hussein na waitifaki wake walidhani kwamba, muda mfupi tu baada ya kuivamia ardhi ya Iran wangeliweza kuuangusha mfumo mchanga wa Kiislamu hapa nchini. Hata hivyo kusimamam kidete wananchi na mapambano ya wapiganaji shupavu wa Kiislamu wa Iran yalibatilisha njama zao na jeshi vamizi la Iraq likalazimika kurejea nje ya mipaka ya Iran baada ya kushindwa mtawalia. 

Siku kama ya leo miaka 12 iliyopita utawala wa Kizayuni wa Israel ulilazimika kuondoka Ukanda wa Ghaza magharibi mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Eneo la Ukanda wa Ghaza lilikaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel wakati wa vita kati ya Waarabu na utawala huo mwaka 1967. Wanajeshi na walowezi wa Kizayuni walikataa kuondoka katika Ukanda wa Ghaza licha ya kutiwa saini makubaliano ya mapatano kati ya Tel Aviv na Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) mwaka 1993 na kuundwa serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ambayo inapaswa pia kulisimamia eneo la Ukanda wa Ghaza.

Askari wa Kizayuni wakiondoka kwa madhila eneo la Ukanda wa Ghaza

 

Tags