Jumamosi, Juni 16, 2018
Leo ni Jumamosi, tarehe Pili Shawwal mwaka 1439 Hijria Qamaria, inayosadifiana na tarehe 16, Juni mwaka 2018 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 42 iliyopita wananchi wa Soweto huko Afrika Kusini walianza harakati za mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi wa makuburu. Katika kipindi hicho Afrika Kusini ilikuwa ikitawaliwa na wazungu wachache waliodhibiti kila kitu na sheria zilizokuwa dhidi ya binadamu. Juni 16 mwaka 1976 maelfu ya wanafunzi wazalendo walifanya maandamano makubwa kupinga sera za kibaguzi katika sekta ya elimu ambayo yalikabiliwa na ukandamizaji mkubwa wa utawala wa kibaguzi. Mamia ya raia waliuawa na wengine kujeruhiwa.
@@@@@@@@@@
Siku kama ya leo miaka 74 iliyopita, yaani sawa na tarehe 16 Juni mwaka 1944, wanajeshi wa majini wa Marekani waliaza kushambulia kwa mabomu miji ya Japan sambamba na kuulenga mji wa Fokula ulioko kusini mwa nchi hiyo. Hayo yalijiri wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Aidha mashambulizi hayo yalifanyika kwa lengo la kuilazimisha Tokyo isalimu amri. Katika mashambulizi hayo makumi ya maelfu ya raia wa Japan waliuawa na kujeruhiwa, sambamba na kuangamizwa viwanda na mashamba ya nchi hiyo. Vita hivyo vilipelekea Marekani kushambulia kwa mabomu ya nyuklia miji miwili ya Japan ya Hiroshima na Nagasaki mwezi Oktoba mwaka 1945.

@@@@@@@@@@
Siku kama ya leo miaka 55 iliyopita sawa na tarehe 16 Juni 1963, Valentina Tereshkova mwanamke wa kwanza duniani mwanaanga kutoka Russia, alianza safari yake ya angani kwa kutumia safina ya anga iliyoitwa Vostok-6. Mwanake huyo alitua katika orbiti ya ardhi wakati ambao Valery Bykovsky mwanaanga mwingine wa Russia alipokuwa akijishughulisha pia kuzunguka dunia. Safari ya Tereshkova katika anga za juu ilifanyika miaka miwili baada ya safari ya Yuri Gagarin ambayo ilikuwa ya kwanza kufanywa na mwanadamu katika anga hizo. Katika muda wa masaa 70 na dakika 50 aliyokuwa katika anga za juu, Tereshkova alizunguka dunia mara 48.
@@@@@@@@@@
Na siku kama ya leo miaka 835 iliyopita, alifariki dunia Abubakar Naqash, msomi wa Qur’an na hadithi mashuhuri wa Iraq. Akiwa kijana mdogo, Naqash alifanya safari mjini Baghdad na kupata kusoma elimu ya dini kwa maulama wakubwa wa zama hizo. Baada ya hapo Abubakar alifanya safari katika nchi tofauti za Kiislamu kwa ajili ya kufanya utafiti katika uga wa maarifa ya dini hususan hadithi. Msomi huyo alikuwa mashuhuri katika zama zake kwa kusoma Qur’an na kunukuu hadithi. Ibn Nadim, mwanahistoria maarufu wa Kiislamu aliyeandika kitabu cha al-Fahrast, alichukua athari nyingi kutoka kwa Abubakr Naqash.