Apr 30, 2019 04:09 UTC
  • Jumanne, 30 Aprili, 2019

Leo ni Jumanne tarehe 24 Sha'aban 1440 Hijria mwafaka na tarehe 30 Aprili 2019 Miladia.

Siku ya leo ya tarehe 10 Ordibehesht inatambulika katika kalenda ya Iran kuwa ni Siku ya Taifa ya Ghuba ya Uajemi. Siku hii imepewa jina la Siku ya Taifa ya Ghuba ya Uajemi kutokana na baadhi ya wanaoichukia Iran kufanya upotoshaji wa historia na kuyapa majina mengine Ghuba ya Uajemi. Jina la Ghuba hii katika lugha mbalimbali ni tarjuma ya neno Ghuba ya Uajemi au Bahari ya Pars. Ghuba ya Uajemi inahesabiwa kuwa ya tatu kwa ukubwa duniani baada ya Ghuba ya Hudson na Ghuba ya Mexico. Kutokana na kuweko  utajiri wa mafuta na gesi katika Ghuba ya uajemi na maeneo yake ya pwani, eneo hili lina umuhimu mkubwa kimataifa. Kwa kuzingatia utambulisho wa kiutamaduni na kihistoria wa taifa la Iran, Baraza Kuu la Mapinduzi ya Utamaduni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, liliitangaza siku ya leo ambayo inakumbusha tukio la kuwaondoa Wareno kutoka lango la Hormuz, kuwa Siku ya Taifa ya Ghuba ya Uajemi.***

Ghuba ya Uajemi

 

Miaka 242 iliyopita katika siku kkama ya leo, alizaliwa Carl Friedrich Gauss mwanahisabati na mnajimu mashuhuri wa Kijerumani. Mama yake Gauss ndiye aliyemshawishi mno mwanawe ajikite zaidi katika somo la hisabati, na hatimaye mtoto huyo alitabahari kwenye fani hiyo. Msomi huyo wa hisabati na mnajimu mashuhuri wa Kijerumani alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.***

Carl Friedrich Gauss

 

Miaka 74 iliyopita, vilimalizika Vita vya Pili vya Dunia barani Ulaya baada ya kutekwa mji wa Berlin. Siku hiyo vikosi vya Jeshi Jekundu vilingia Berlin kudhibiti mji huo ambao ulikuwa makao makuu ya dikteta wa Ujerumani Adolf Hitler. Baada ya Jeshi Jekundu kukaribia makazi ya Hitler yaliyokuwa chini ya ardhi, dikteta huyo aliamua kujinyonga pamoja na mpenzi wake, Eva Braun. Hitler ni miongoni mwa wanzilishi wa Vita vya Pili vya Dunia ambavyo vilisababisha vifo vya watu milioni 50. Baada ya kutundika maiti za Mussolini na wenzake, Hitler aliingia kwenye makazi yake chini ya ardhi na kufunga ndoa na mpenzi wake wa zaidi ya muongo mmoja Eva Braun, na masaa machache baadaye wote wawili walijinyonga baada ya Jeshi Jekundu kuteka sehemu kubwa ya mji wa Berlin. ***

Adolph Hitler

 

Katika siku kama ya leo miaka 49 iliyopita, mwandishi na msanii wa uchoraji wa zama hizi wa Iran, Ustadh Ismail Ashtiyani alifariki duunia. Baada ya masomo ya msingi na upili, Ustadh Ashtiyani alijifunza sanaa ya uchoraji kwa msanii mashuhuri wa zama hizo Kamalul Mulk. Mwaka 1307 Hijria Shamsia alishika wadhifa wa mkuu wa Chuo cha Sanaa cha Darul Funun. Miongoni mwa vitabu vyake ni pamoja na diwani ya mashairi, Kumbukumbu ya Ulaya na Historia ya Kamalul Mulk. ***

Ustadh Ismail Ashtiyani

 

Na miaka 39 iliyopita katika siku kama ya leo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikata uhusiano wake na Misri. Amri ya kukatwa uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu na Misri ilitolewa na hayati Imam Ruhullah Khomeini baada ya Rais wa wakati huo wa Misri, Anwar Saadat kutia saini makubaliano ya aibu na fedheha ya Camp David na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusaliti malengo ya Wapalestina. Kutiwa saini makubaliano hayo ilikuwa hatua ya kuhalalisha uvamizi wa Wazayuni dhidi ya Palestina na kusaliti haki za Wapalestina waliokuwa wakipambana na utawala haramu wa Israel na vilevile kupuuza maslahi ya Umma wa Kiislamu. Baadaye kiongozi huyo wa Misri alitiwa adabu na shujaa, Khalid Islambuli aliyemmiminia risasi na kumuua kutokana na usaliti huo. ***

Muhammad Anwar Sadat

 

Tags