Sep 12, 2020 00:41 UTC
  • Jumamosi, 12 Septemba, 2020

Leo ni Jumamosi tarehe 23 Mfunguo Nne Muharram 1442 Hijria mwafaka na tarehe 12 Septemba 2020 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 233 iliyopita,  aliaga dunia Allamah Mulla Muhammad Mahdi Naraqi, mwanazuoni na msomi mkubwa wa Kiislamu. Baada ya kuhitimu masomo ya awali nchini Iran, Mahdi Naraqi alielekea Najaf nchini Iraq kwa lengo la kuzidisha elimu na alipata elimu kwa walimu mashuhuri wa zama hizo. Baada ya hapo Allamah Mulla Mahdi Naraqi alianza kufanya utafiti, kufundisha na kuandika vitabu. Miongoni mwa vitabu mashuhuri vya Allamah Naraqi ni "Jaamiul Sa'adat" na " Anisul Muwahhidin". ***

Allamah Mulla Muhammad Mahdi Naraqi,

 

Miaka 123 iliyopita, inayosadifiana na 12 Septemba 1897, Irene Joliot- Curie mtaalamu wa Fizikia na Kemia wa Ufaransa, alizaliwa katika mji wa Paris. Baada ya kufanya utafiti wa muda mrefu, Irene Joliot- Curie alifanikiwa kuvumbua mada za radioactive.***

Irene Joliot- Curie

 

Miaka 113 iliyopita katika siku kama ya leo, aliaga dunia msomi wa elimu wa Fikihi wa Kishia Ayatullah Haj Mirza Ibrahim Khui. Msomi huyo ambaye ni mashuhuri kwa jina la Allama Khui, alizaliwa mwaka 1210 katika mji wa Khui. Baada ya kumaliza masomo yake ya msingi nay a kati ya idini alielekea katika Hawza ya Najaf nchini Iraq. Akiwa huko Allama Khui alihudhuria darsa na masomo ya waalimu watajika wa zama hizo kama Sheikh Murtadha Ansari na kufanikiwa kuzikwea daraja za kielimu. ***

Ayatullah Haj Mirza Ibrahim Khui.

 

Siku kama ya leo miaka 46 iliyopita, nchini Ethiopia kulitokea mapinduzi yaliyopelekea kuondolewa madarakani utawala wa Haile Selassie. Haile Selassie alizaliwa mwaka 1892 nchini Ethiopia. Awali alikuwa mkuu wa mikoa kadhaa nchini humo na baadaye akawa mrithi wa kiti cha ufalme. Mwaka 1930 alishika hatamu za uongozi wa Ethiopia akiwa mfalme wa nchi hiyo. Awali alifanya jitihada kubwa za kuyaunganisha makabila ya Ethiopia kwa shabaha ya kuyadhibiti. Haile Selassie aliwaajiri wataalamu wa kigeni na kuanza kufanya marekebisho ya kidara hatua kwa hatua. Alikomesha utumwa, akafanya marekebisho ya masuala ya kifedha na kuanzisha mfumo wa mahakama nchini Ethiopia. Hata hivyo mashambulio ya Italia dhidi ya Ethiopia mwaka 1935 yalisitisha mpango wake huo na alibakia nje ya nchi hadi mwaka 1941 aliporejea nchini kwa msaada wa Waingereza na kutwaa tena madaraka. Aliendeleza marekebisho yake ambayo zaidi yalijikita katika mji mkuu Addis Ababa na mambo yasio ya msingi huku sehemu kubwa ya Waethiopia wakikosa suhula za kimsingi za maisha. Selassie alikuwa tegemeza sana kwa nchi za Magharibi. Tarehe 12 Septemba mwaka 1974 Selassie aliondolewa madarakati katika mapinduzi yaliyofanywa na wanajeshi wa nchi hiyo na mwaka mmoja baadaye utawala wa kifalme ulikomeshwa kabisa nchini Ethiopia.

Haile Selassie

 

Katika siku kama ya leo miaka 40 iliyopita, nchini Uturuki kulitokea mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Jenerali Kenan Evren na kupelekea kuondolewa madarakani Waziri Mkuu Suleyman Demirel na kisha kuundwa serikali ya kijeshi. Kuibuka kashfa ya ufisadi wa fedha na kuendelea hali ya kulegalega kisiasa na kijamii nchini Uturuki kulipelekea kutokea mgogoiro wa kiuchumi ambapo hatimaye katika siku kama ya leo Jenerali Kenan aliyekuwa mkuu wa majeshi alifanya mapinduzi. Baada ya mapinduzi hayo, Jenerali Kenan akiwa pamoja na Baraza la watu sita walishika hatamu za uongozi wa nchi. Mbali na Waziri Mkuu kuondolewa madarakani kulitolewa amri pia ya kuvunjwa Bunge sambamba na kupigwa marufuku shughuli za vyama vya siasa na nchi ikawa inatawaliwa na serikali ya kijeshi.

Jenerali Kenan Evren

 

Na katika siku kama ya leo miaka 15 iliyopita, Haram takatifu ya Maimamu al Hadi na Hassan al-Askari katika mji wa Samarra nchini Iraq, ziliharibiwa vibaya kwenye mashambulizi kadhaa ya miripuko ya mabomu yaliyofanywa na makundi ya kigaidi na kusababisha hasara kubwa za mali na watu. Maimamu hao ni wajukuu wa Mtume Bwana Mtume Muhammad SAW na walikuwa na nafasi kubwa ya kielimu na wacha-Mungu wangu katika zama zao. Kitendo cha kuharibiwa eneo hilo kiliwakasirisha mno Waislamu duniani hususan wafuasi wa Ahlul Bait wa Mtume (saw). Shambulio hilo lilifanyika kwa lengo la kuzusha ufa katika safu za Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni nchini Iraq.aram takatifu ya Maimamu al Hadi na Hassan al-Askari katika mji wa Samarra nchini Iraq.

Tags