Jun 08, 2021 21:53 UTC
  • Jumatano tarehe 9 Juni mwaka 2021

Leo ni Jumatano tarehe 28 Shawwal 1442 Hijria sawa na Juni 9 mwaka 2021.

Siku kama ya leo miaka 1953 iliyopita inayosadifiana na tarehe 9 Juni mwaka wa 68 Milaadia, Mfalme Nero Claudius Caesar mtawala katili na aliyemwaga damu nyingi wa Rome alijiua, baada ya kuishi kwa miaka 31 na kutawala kwa maiaka 14. Si vibaya kuashiria hapa kwamba Nero aliasiliwa na mjomba wake Mfalme Claudius aliyekuwa mtawala wa kwanza wa Rome. Lakini Nero alimpa sumu mfalme huyo na kuchukua nafasi yake baada ya kufa. Mfalme huyo katili na wa mwisho wa Rome, wakati wa utawala wake aliwaua watu wengi wa familia yake akiwemo mama yake, mkewe, kaka yake na ndugu zake wengine. Pia aliwaua wananchi wake wengi. Aliwaua kwa umati Wakiristo pamoja na kuuchoma moto mji wa Rome.

نرون

Siku kama ya leo miaka 969 iliyopita alizaliwa Sanai Ghaznawi Hakim Abul-Majd Majdud ibn Ādam Sanai Ghaznavi, malenga, tabibu na mwanairfani mkubwa wa Iran mjini Ghazni. Ghaznavi alianza kusoma mashairi ya kuwasifu watawala akiwa bado kijana mdogo. Hata hivyo muda mfupi baadaye aliachana na mwenendo huo na kuanza kusomea elimu ya irfan (ya kumjua Mwenyezi Mungu). Kuanzia wakati huo alianza kuishi maisha ya kuwatumikia wananchi sambamba na kusoma mashairi ya kuwakosoa watawala dhalimu na mafisadi. Alianzisha pia mfumo wa aina yake katika usomaji wa mashairi. Miongoni mwa athari za Sanai Ghaznawi ni pamoja na kitabu cha 'Hadiqatul-Haqiqah' ambacho kina muundo wa mashairi na ndani ya kitabu hicho malenga huyo mkubwa ameweka wazi fikra zake za kimaadili na irfani. Vitabu vya 'Elahi Nameh' 'Karnameh Balkh' na 'Twariqut-Tahqiq,' ni miongoni mwa athari za Sanai Ghaznawi.

حکیم سنایی غزنوی

Miaka 136 iliyopita muwafaka na leo, jeshi la Ujerumani lilivamia ardhi ya Togo huko magharibi mwa Afrika. Wakati huo maeneo ya pwani ya Togo yalikuwa sehemu bora kwa watu wa Ulaya kwa ajili ya biashara ya utumwa. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana Togo imekuwa maarufu kwa jina la "Pwani ya Utumwa." Wakoloni wa Ujerumani waliendelea kuikalia kwa mabavu ardhi ya Togo hadi wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. Baada ya hapo Togo ilikoloniwa na Wafaransa na Waingereza. Nchi hiyo ilipata uhuru mwaka 1960.

توگو

Siku kama ya leo miaka 59 iliyopita moto mkubwa ulitokea katika Chuo Kikuu cha Algiers mji mkuu wa Algeria. Moto huo ulichoma zaidi ya nakala laki tano za vitabu vyenye thamani kubwa zilizokuwa kwenye maktaba ya chuo hicho. Asilimia kubwa ya vitabu vilivyoungua vilikuwa miongoni mwa marejeo muhimu na nadra. Chuo Kikuu cha Algiers na maktaba yake vilichomwa moto na jeshi la siri la Ufaransa nchini Algeria. Jeshi hilo la siri liliundwa na askari wa Ufaransa waliokuwa wakipinga suala la kupewa uhuru Algeria. Moto huo ulikuwa miongoni mwa makumi ya mioto kadhaa iliyotokea katika siku hiyo nchini Algeria na mingi ilisaabishwa na jeshi la siri la Ufaransa.

ساختمان کنونی کتابخانه ملی الجزایر

Siku kama ya leo miaka 53 iliyopita, alifariki dunia Ayatullah Sayyid Muhammad Hassan Ilahi Tabatabai, mmoja wa maulamaa na wataalamu wa elimu ya irfani. Sayyid Muhammad Tabatabai alizaliwa Tabrizi huko kaskazini mwa Iran mwaka 1325 Hijiria. Akiwa na miaka 19 alielekea  Najaf, Iraq akiwa na kaka yake mkubwa, Allamah Muhammad Hassein Tabatabai na kusoma elimu ya dini mjini hapo. Baada ya kutabahari katika elimu za Kiislamu alirejea eneo alikozaliwa la Tabriz na kujishughulisha na malezi na kutoa elimu kwa wanafunzi. Mwanazuoni huyo ameandika vitabu kadhaa kikiwemo kile cha Uhusiano wa Kimaanawi Baina ya Roho na Sauti. 

سید محمدحسن الهی طباطبایی