Jun 09, 2022 23:18 UTC
  • Ijumaa, Juni 10, 2022

Leo ni Ijumaa mwezi 10 Mfunguo Pili Dhulqaad 1443 Hijria, sawa na tarehe 10 Juni, 2022 Milaadia.

Siku kama ya leo miaka 1054 iliyopita iliyosadifiana na mwezi 10 Mfunguo Pili Dhulqaad mwaka 389 Hijria, utawala wa kifalme wa Wasamani (Samanian - Samanid) ulisambaratika nchini Iran baada ya kutawala kwa muda wa miaka 128 katika eneo ambalo wakati huo likijulikana kwa jina la Khurasan au Transoxiana ambalo ni sehemu ya katikati ya Iran na leo. Ufalme wa ukoo wa Samanian ulisambaratishwa na mtu aliyejulikana kwa jina la Ilik Khan ambaye alikuwa mtumwa wa Warutuki. Alifanikiwa kusambaratisha ufalme huo kutokana na nguvu na ushawishi wake mkubwa ndani ya ukoo wa kifalme wa wasamani. Wakati walipokuwa na nguvu, watawala wa Kisamani walitilia mkazo sana kujenga miji ya utawala wao. Walilipa umuhimu mkubwa suala la kueneza elimu na fasihi na walikuwa wakiwakirimu sana wasomi, maulamaa na watu wa fasihi na mashairi. Utawala huo ulijenga vituo vingi vya kielimu katika maeneo tofauti ya Asia ya Kati na Khurasan yaani kaskazini mashariki mwa Iran ya leo. Ufalme wa ukoo wa Buyid (Aal Buyeh) wa Waturuki ndio ulioanza kutawala Iran baada ya kusambaratika ufalme wa ukoo wa Wasamani.

Eneo la utawala wa wafalme wa Wasamani (Samanian - Samanid)

 

Miaka 617 iliyopita katika siku inayosadifiana na hii ya leo Abu Abdullah Muhammad bin Muhammad maarufu kwa jina la Sibt al Mardini, mnajimu na mwanahisabati wa Kiislamu alizaliwa huko Damascus. Wanahistoria wamesajili vitabu karibu 42 kwa jina la msomi huyo na baadhi ya vitabu hivyo vimehifadhiwa hadi leo hii. Moja kati ya athari za Sibt al Mardini ni kitabu chake cha hisabati kinachojulikana kwa jina la Daqaiqul Haqaaiq.

S

Sibt al Mardini

 

iku kama ya leo miaka 232 iliyopita yaani tarehe 10 Juni 1790 vikosi vya jeshi la Uingereza viliivamia ardhi ya Malaya inayojulikana hii leo kama Malaysia. Wakati huo Uholanzi ilikuwa ikiikoloni Malaya na kupora utajiri mkubwa wa nchi hiyo wa madini ya bati. Uholanzi ilianza kuondoka katika ardhi ya Malaya baada ya jeshi la Uingereza kuingia nchini humo na mwaka 1824 ilikubali kuiachia Uingereza ardhi hiyo kwa sharti kwamba nayo iachiwe Indonesia ambayo ilikuwa na umuhimu mkubwa kwa Uholanzi. Malaysia ilijipatia uhuru wake mwaka 1957 na Indonesia mwaka 1956.

Bendera ya Malaysia

 

Siku kama ya leo miaka 210 iliyopita, vilianza vita vya Marekani na Uingereza. Miongoni mwa matukio muhimu ya historia ya Marekani katika nusu ya kwanza ya karne ya 19 ni vita hivyo vilivyoendelea kwa miaka miwili. Sababu ya kuanza vita hivyo inasemekana ni kuzingirwa Ufaransa na Uingereza kutokea baharini na kuzuiwa safari za meli za Marekani katika maji yanayozunguka nchi za Ulaya. Lakini pamoja na hayo Marekani ilikuwa na sababu nyingine za kuanzisha vita hivyo, muhimu kati ya hizo ilikuwa ni madai ya uungaji mkono wa siri wa Uingereza kwa Wahindi Wekundi wa Marekani dhidi ya serikali kuu ya nchi hiyo. Kufuatia vita hivyo, tarehe 18 Juni 1812 wanajeshi wa Marekani walivamia vituo na mali za Uingereza huko Canada na kuuteketeza mji wa Toronto. Vita hivyo vilipamba moto kiasi kwamba mwezi Agosti 1814 Uingereza ilituma askari wake katika pwani ya mashariki ya Marekani na kuendesha vita hadi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Washington DC. Hatimaye mazungumzo ya amani baina ya nchi mbili hizo yalitiwa saini huko Ubelgiji na kupelekea kusimamishwa vita hivyo mwezi Disemba mwaka huhuo wa 1814.

Bendera za Marekani na Uingereza

 

Siku kama ya leo miaka 99 iliyopita, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 73 Pierre Loti, mwandishi mkubwa wa Ufaransa. Baada ya kuhitimu masomo yake ya msingi na ya juu, alijiunga na kikosi cha majini katika jeshi la Ufaransa sambamba na kuhudumia nyadhifa kubwa jeshini. Ni wakati huo ndipo alipoanzisha shughuli zake za fasihi huku akieneza machapisho yake. Muda mfupi baadaye Pierre Loti alipata umshuhuri ambapo mwaka 1891 aliteuliwa kujiunga na kituo cha utamaduni nchini humo. Baada ya hapo alifanya safari mashariki ya mbali, safari za baharini na Mashariki ya Kati na kupata kuandika kuhusu mambo mbalimbali duniani. Aidha Loti alifika nchini Iran na kuandika kitabu kuhusiana na mambo ya kuvutia ya mjini Isfahani. Pierre Loti aliacha athari mbalimbali ambazo baadhi zipo hadi leo katika maktaba za nchini Ufaransa.

Pierre Loti

 

Siku kama ya leo miaka 52 iliyopita, aliuawa shahidi Ayatullah Sayyid Muhammad Reza Saeedi, mmoja wa wasomi wakubwa na wanamapambano wa Iran baada ya kuteswa kwa muda mrefu katika mojawapo ya jela za utawala wa kitwaghuti wa Shah. Alielekea mjini Qum na kujiunga na chuo cha kidini cha mji huo na kupata elimu kwa maulama wakubwa akiwemo Ayatullahil-Udhma Borujerdi na Imamu Khomein (MA). Baada ya mwamko wa mapinduzi ya wananchi Waislamu nchini Iran, tarehe 15 Khordad 1342 Hijiria, alidizisha harakati zake dhidi ya utawala wa kidikteta wa Shah. Katika uwanja huo, Ayatullah Sayyid Muhammad Reza Saeedi aliufanya msikiti wake kuwa ngome ya kuwazindua na kuwahamasisha wananchi hususan vijana, na hotuba zake nyingi zilijikita katika kufichua njama chafu za ukoloni na jinai za utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya watu madhlumu wa Palestina. Ni kwa sababu hiyo ndio maana alikamatwa mara kadhaa na kufungwa jela. Hata hivyo vitendo hivyo vya utawala wa Shah havikuweza kuathiri hata kidogo katika azma ya mwanazuoni huyo mtajika wa Kiislamu. Miongoni mwa athari za Ayatullah Sayyid Muhammad Reza Saeedi ni pamoja na kitabu cha ‘Umoja wa Kiislamu’ ‘Uhuru wa Mwanamke’ na ‘Kazi na Uislamu.’

Ayatullah Sayyid Muhammad Reza Saeedi

 

Katika siku kama ya leo miaka 41 iliyopita, Bani Sadr Rais wa kwanza wa Iran baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliuzuliwa na Imam Khomeini wadhifa wa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote kutokana na kusalitii nchi. Tangu awali baada ya kuchaguliwa kuwa Rais, Bani Sadr alikumbwa na kiburi na ghururi na akawa anafuatilia suala la kuwaweka kando wanamapinduzi watiifu kwa Imam Khomeini, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Bani Sadr pia alikuwa akishirikiana na makundi yaliyokuwa yakipinga Mapinduzi ya Kiislamu. Vilevile alikwamisha utendaji wa serikali kutokana na kukwepa kwake kumkubali Waziri Mkuu Muhammad Rajai mmoja wa wanamapambano mashuhuri aliyekuwa amechaguliwa na Bunge kwa wingi wa kura. Ukwamishaji huo wa Bani Sard ulifikia kileleni katika vita vya kichokozi vya Iraq dhidi ya Iran na kupelekea miji mingi ya Iran katika kipindi hicho cha vita kukaliwa kwa mabavu na utawala wa dikteta Saddam Hussein. Hatimaye katika siku kama ya leo, Imam Khomeini alimuuzulu Bani Sadr cheo cha Amiri Jeshi Mkuu. Siku chache baadaye Bunge lilipasisha kwa wingi wa kura mpango wa kutokuwa na imani na uwezo wa kisiasa Rais huyo.

Bani Sadr

 

Na miaka 22 Iiyopita siku kama ya leo, Hafidh Assad rais wa wakati huo wa Syria aliaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alizaliwa mwaka 1930. Aliteuliwa kuwa kamanda wa kikosi cha anga cha Syria mwaka 1964 na kuwa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo miaka mitatu baadaye. Aliipindua serikali ya wakati huo ya Syria mwaka 1970 na kuchukua uongozi wa nchi hiyo na kisha kuteuliwa kuwa kiongozi wa chama cha Baath. Assad aliimarisha jeshi la nchi hiyo kiasi kwamba mwaka 1973 alifanikiwa kurejesha sehemu ya milima ya Golan iliyotekwa na kukaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel katika vita vya 1967. Siasa muhimu za Assad zilikuwa ni za kutofanya mapatano na utawala huo ghasibu.

Hafidh Assad

 

Tags