May 26, 2023 11:16 UTC
  • Mchango wa Maulamaa wa Kishia Katika Uislamu (69)

Ni matumaini yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji popote pale mlipo na karibuni katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Mchango wa Maulamaa wa Kishia Katika Uislamu, ili tuweze kwa pamoja kufungua ukurasa mwingine katika kurasa za historia ya Maulamaa na wanazuoni wa Kishia pamoja na mchango wao katika Uislamu.

Kipindi chetu kilitangulia kilimzungumzia mmoja wa wanafunzi maalumu wa Sheikh Murtadha Ansari yaani Mirza Habibullah Rashti. Tulieleza kwamba, Habibullah Rashti alizaliwa 1234 Hijria katika mji wa Gilan Iran katika eneo linalojulikana kwa jina la Amlesh. Mababu zake walikuwa na asili ya Qochan na baba yake Muhammad Ali Qochani Gilani alikuwa akihesabiwa kuwa mmoja wa watu na shakhsia mahiri na wakubwa wa Gilan. Tuliona jinsi aliavyoanza harakati za kupinga dhulma akiwa bado kijana mdogo. Tuliashiria pia jinsi alivyofanikiwa kufikia daraja ya Umarjaa akiwa na umri wa miaka 25 tu. Sehemu ya 69 ya kipindi chetui cha leo itatupia jicho kwa mukhtasari maisha na mchango wa Jihangiri Khan Qashqai alimu na msomi mahiri wa Kishia. Nina wingi wa matumaini kuwa mtakuwa nami hadi mwisho wa kipindi hiki. Karibuni.

 

Jahangiri Khan Ghashghaei alizaliwa 1243 Hijria mwafaka na 1828 Miladia katika moja ya viunga vya mji wa Isfahan nchini Iran. Jahangiri kama walivyo0kuwa watoto wengine wa eneo la Ghashghaei alijifunza malema kupanda farasi na kulenga shabaha. Kutokana na kuonekana kuwa na kipaji, akili na maarifa ya hali ya juuu, baba yake aliamuandalia mazingira ya kujifunza masomo ya msingi. Hakusoma masomo hayo kwa kwenda shule au katika maktaba kama ilivyokuwa ikijulikana hapo kale, bali kwa kuletewa mwalimu nyumbani. Akiwa na umri wa miaka 40,

Jahangiri alifahamiana na mmoja wa shakhsia, wasomi na wanazuoni mahiri katika zama z\hizo ambaye alikuwa mtu wa mashairi. Alimu huyo alimshajiisha Jahangiri Khan Ghashghaei na kumshauri ajiunge na shule kwa ajili ya masomo kwani ana kipaji cha hali ya juu cha ufahamu. Hatimaye Jahangiri Khan akajiunga na chuo cha Sadr cha Isfahan na kuanza kujishughulisha na maasomo.

Katika zama hizo za kale, ilikuwa ada kwamba, katika madrasa na vyuo vya kidini mbali na kufundishwa fikihi na usul kulikuwa kukifundishwa elimu nyingine za nakili kaama hadithi na kadhalika, na elimu za kiakili kama hisabati, tiba na nyinginezo. Daima Maulamaa wa Kishia walikuwa wakizingatia naa kutoa kipaaumbe kwa akili na utumiaji akili. Hii ni kutokana na kuwa, daima Uislamu unawataka wafuasi wake kutumia akili, kutafakari na kutadabari na kuwataka wasikubali jambo pasi na kulitafakari na kulitia akilini.

Moja ya elimu za kiakili ambazo daima zilikuwa zikizingatiwa na kuupewa umuhimu na shakhsia wakubwa wa Kishia ni falsafa na kutuumia hoja za kiakili kwa ajili ya mafuhumu na maana yaa Qur'ani. Hata hivyo katika kipindi chote cha historia walikuweko watu ambao walikuwa na mtazamo finyu na fikra zisizo na upeo wa mbali, ambao walikuwa wakiyatazama mafundisho wa dini katika hali yake ya dhahiri tu. Watu hawa hawakuwa wakilitambua na kuliamini suala la kutakafari na kuangalia mambo kwa batini na undani zaidi na hivyo kutumia akili. Walikuwa wakiamini kwamba, hilo haliwezi kufanywa na watu wa kawaida bali ni mahususi na maalumu kwa watu maalumu kama Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (as) na wengine wanapaswa kufuata tu bila ya kutakafari.

Chuo cha Sadr Isfahan

 

Katika kipindi chote cha maisha ya kijamii ya Waislamu, kulikuweko na duru katika historia ambayo kutokana na sababu za kisiasa na kijamii watu wenye fikra finyu na mtazamo wa juu walikuwa ndio waliowengi katika jamii. Kipindi hiki cha historia, katika vyuo vya kidini, taaluma ya falsafa lilikuwa jambo geni na lililokuwa limehamwa. Si hivyo tu bali baadhi ya watu walikwenda mbali zaidi na kutoa hukumu ya kwamba, falsafa ni ukafiri. Kipindi ambacho Jahangir Khan Ghashghaei alipoingia katika chuo cha Isfahan akiwa na kipaji na upeo ule wa hali ya juu, kilikuwa ndio kile kipindi cha falsafa kuhamwa na kuonekana kuwa ni kitu kigeni na cha ajabu.

Katika hali ambayo, kusoma falsafa na kujihusisha nayo ni jambo ambalo lilifikia  hatua ya kutambuliwa kuwa ni ukafiri na wqatu waliokuwa na shauku na mapenzi na taaluma ya falsafa walilazimika kujifunza kwa siri elimu hii. Jahangir Khan Ghashghaei akaondokea kuwa na mapenzi na falsafa ya Mulla Sadra. Maktaba hii ya falsafa inajulikana kwa jina la Hekmat al-Mutaaliya. Hii ni kutokana na kuwa, imechanganya baina ya irfani na falsafa. Hivyo basi, mbali na kujifunza fikihi, usul, fasihi ya lugha ya kiarabu na elimu nyingine kama hisabati, tiba na nujumu, alijifunza kwa bidi pia elimu ya falsafa kwa Muhammad Reza Qumshei, mmoja wa wasomi mashuhuri wa elimuu ya falsafa katika zama hizo mjini Isfahan.

Kutokana na kipaji na bidi aliyokuuwa nayo, kwa haraka mno, Jahangir Khan Ghashghaei alikkwea daraja za elimu na akaanza kufundisha katika Chuo Kikkuu cha Kidini (Hawza) katika mji wa Isfahan. Mbali na kufundisha elimu kama fikihi, usul na akhlaq alikuwa akiwafundisha pia wanafunzi wake elimu ya falsafa kwa mbionu na njia ya kuvutia mno. Jahangir Khan Qashqai alikuwa amebobea mno katika elimu hiyo kiasi kwamba, hatua kwa hatua mtazamo wa watu wote kuhusiana na elimu ya falsafa ukabadilika na hivyo kuwafanya wapinzani wa elimu hiyo kugeuka na kuwa jamii ya wachache.

 

Akiwa na lengo la kubainisha masuala mbalimbali ya kifalsafa, Jahangir Khan alikuwa akitumia maneno ya Imam Ali ibn Abi Twalib (as) na alikuwa akifuundisha somo la Nahaj al-Balagha (Njia ya Balagha) kwa kuuchanganya na elimuu ya faklsafa. Ujanja na ubunifu wake huu kwa sehemu kubwa ulipelekea elimu ya falsafa siyo tu kwamba, isituhumiwe kwamba, inapingana na sheria na kuliokoa na hilo, bali mafakkihi na wanazuoni wa elimu ya fikihi nao pia wakaonyesha kuwa na mapenzi na elimu hii na kuityambua kwamba, ni chimbuuko la fadhila na ukubwa. Hakim Jahangir Khan mpaka mwishoni mwa umri wake hakuvaa mavazi ya  wanazuoni wa kidini na katika mahafali zote alikuwa akihudhuria na zilezile nguo zake za kawaida kabisa zilizokuwa na kila ishara ya tawadhui na unyenyekevu. Alikuwa akijitambua kuwa, hastaki mavazi hayo ya Mtume.

Msomi huyu amelea na kutoa wanafunzi wengi walioondokea kuwa wanazuoni mahiri katika zama zao. Miongoni mwao ni Ayatullah Borujerdi, mtu ambaye baadaye aliondokea kuwa Marjaa mkubwa wa Kishia ulimwenguni.

Mahali alipozikwa Jahangir Khan Ghashghaei

 

Baada ya miaka 45 ya kutafuta elimu, hatimaye Jahangir Khan Ghashghaei aliaga dunia mwaka 1910 iliyosadifiana na mwezi mtukufu wa ramadhani akiwa na umri wa miaka 85 na kuzikwa huko Isfahan moja ya miji ya Iran

Wapenzi wasikilizaji muda wa kipindi chetu kwa juma hili umefikia tamati, tukutane tena juma lijalo saa na wakati kama wa leo. Basi hadi tutakapokutana tena wakati huo, ninakuageni nikikutakieni kila la kheri.

Wassalaam Warahmatullahi  Wabarakaatuh.