Jun 02, 2023 01:31 UTC
  • Ijumaa, Juni 02, 2023

Leo ni Ijumaa tarehe 13 Mfunguo Pili Dhulqaada 1444 Hijria sawa na tarehe Pili Juni 2023 Milaadia.

Siku kama ya leo miaka 678 iliyopita, alifariki dunia Qutbuddin Muhammad Razi. Razi alizaliwa katika eneo la Varamin kwenye viunga vya mji wa Rey na alipata umashuhuri kwa jina la Razi kwa kuwa alikulia katika mji huo. Qutbuddin Muhammad Razi alikuwa mwanafunzi mkubwa wa Allamah Hilli. Kwa kipindi fulani aliwatumikia Sultan Abu Said na waziri wake Khaja Ghiyathuddin Muhammad na aliandika viwili vya 'Sharhu al-Shamsiyyah' na 'Sharhul Matwaali' kwa jina la waziri huyo.' Baada ya kufariki dunia Sultan Abu Said, Qutbuddin Muhammad Razi alielekea Sham na alifariki dunia mjini Damascus.

Siku kama ya leo miaka 416 iliyopita alifariki dunia Ayatullah Mirza Muhammad Isterabadi, mtaalamu wa sheria za Kiislamu na elimu ya theolojia. Ayatullah Mirza Muhammad Bin Ali Bin Ibrahim Isterabadi alikuwa mmoja wa maulama wakubwa wa Kiislamu. Awali alikuwa akiiishi mjini Najaf, Iraq na baadaye alielekea Makkah na kufanya makazi mjini hapo. Isterabadi ni kati ya watu wanaoelezwa kuwa waliopata sharafu ya kukutana na Imam wa zama (af). Msomi huyo aliandika vitabu juu ya wapokezi wa hadithi kikiwemo kitabu cha 'Tawdhihul-Maqaal' 'Talkhisul-Aqwaal' na 'Manhajul-Maqaal.' Vitabu hivyo vinatambuliwa kuwa vitabu muhimu na chemchemi ya elimu ya wapokezi wa hadithi.

میرزا محمد استرآبادی

Katika iku kama hii ya leo miaka 141 iliyopita alifariki dunia Giuseppe Garibaldi kamanda mzalendo na kiongozi wa harakati ya kuleta umoja wa Italia. Giuseppe alizaliwa mwaka 180 na wakati wa ujana wake alifanya kazi mbalimbali na mwishowe kujiunga na jeshi. Baadaye alichaguliwa kuwa kamanda wa wanaharakati wa kupigania uhuru wa Italia na alifanya jitihada nyingi za kuleta umoja nchini humo. Kwa ajili hiyo alijulikana katika historia ya Italia kama shujaa wa taifa.

Giuseppe Garibaldi

Siku kama ya leo miaka 81 iliyopita, mnamo tarehe Pili Juni mwaka 1942 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, Mjerumani Marshal Erwin Rommel maarufu kwa jina la Mbwa Mwitu wa Jangwani, alianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya jeshi la Uingereza katika maeneo ya kaskazini mwa Afrika. Kabla ya mashambulizi hayo, Waingereza walikuwa wamefanya hujuma nchini Libya na kuitwaa nchi hiyo kutoka mikononi mwa jeshi la Wajerumani wa Kinazi. Hata hivyo mashambulizi ya jeshi la Erwin Rommel ambayo yalidumu kwa kipindi cha mwezi mmoja yaliwawezesha wanajeshi wake kuidhibiti tena Libya na eneo la al Alamein lililoko kaskazini mwa Misri na karibu na bandari muhimu ya Alexandria. Wajerumani walikaribia kuutwaa mfereji wa kistratijia wa Suez lakini mwezi Novemba mwaka 1942 Waingereza wakafanya mashambulizi makubwa dhidi ya jeshi la Erwin Rommel na hatimaye kulishinda.

Siku kama ya leo Miaka 53 iliyopita, Ayatullah Sayyid Muhsin Hakim, mkuu wa kituo cha kidini cha Najaf aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 92. Baada ya kuaga dunia Ayatullah Burujerdi ambaye alikuwa mar'ja' mashuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu, Ayatulah Hakim alichukua nafasi yake na kufuatwa na Waislamu wengi na hasa wa Iraq, kuhusiana na masuala ya kifik'hi. Alipambana vikali na kila kundi au watu waliojaribu kuharibu jina la Uislamu. Fatua yake mashuhuri ya kupinga fikra ya ukomunisti dhidi ya mafundisho ya dini ilileta mabadiliko makubwa nchin Iraq. Fatua hiyo pia ilimpelekea kutoa amri ya kupigana jihadi dhidi ya utawala haramu wa Israel. Ujenzi wa maktaba, shule na vituo vya kidini na kiutamaduni pamoja na uandishi wa vitabu kama vile Mustamsak Urwat al-Wuthqah na Nahjul Faqaha ni miongoni mwa vitabu mashuhuri vilivyoandikwa na mwanazuoni huyo mashuhuri wa Kiislamu.

Ayatullah Sayyid Muhsin Hakim,

Miaka 23 iliyopita katika siku kama ya leo,  sawa na tarehe 12 Khordad mwaka 1379 Hijiria Shamsia, alifariki dunia Hujjatul Islam Sayyid Ali Akbar Abuturabi, mwanzuoni mwenye mwamko na mwanaharakati wa Iran katika ajali ya gari pamoja na baba yake Ayatullah Sayyid Abbas Abuturabi. Hujjatul Islam Sayyid Ali Akbar Abuturabi alizaliwa mwaka 1318, kwa mujibu wa kalenda ya Iran, katika mji wa kidini wa Qum. Alijifunza elimu ya dini kutoka kwa maulamama wakubwa akiwemo Imam Khomeini (M.A). Hujjatul Islam Abuturabi katika mapambano ya kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu mara kadhaa alikamatwa na kuteswa na vibaraka wa Shah. Wakati vya vita vya Iran na Iraq mwaka 1359 alikamatwa mateka na askari wa utawala wa Baath wa Iraq na kufungwa kwa miaka 10 katika jela zenye mateso makali za Iraq. Lakini alivumilia kiasi cha kuwa mashuhuri miongoni mwa mateka wa Iran kwenye jela hizo. Alipoachiliwa huru aliteuliwa kuwa mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya mateka na walioachiliwa huru.

Ali Akbar Abuturabi

 

Tags