-
Cuba yaunga mkono kesi iliyofunguliwa na Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni
Jan 18, 2024 06:01Bruno Rodríguez Parrilla Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba amesema kuwa Havana inaunga mkono mashtaka yaliyowasilishwa na Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu mauaji ya kimbari yaliyofanywa na utawala wa Israel dhidi ya watu wa Gaza.
-
Afrika Kusini kuzishtaki Marekani na Uingereza kwa kuhusika na jinai za kivita za Israel Gaza
Jan 16, 2024 03:35Baada ya Afrika Kusini kuwasilisha kesi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa kuhusika na mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza, mawakili wapatao 50 wa nchi hiyo wanatayarisha mashtaka mengine tofauti dhidi ya serikali za Marekani na Uingereza kwa msingi kwamba, serikali hizo zinahusika katika jinai na uhalifu unaofanywa na jeshi la Israel huko Gaza.
-
"Dunia ina wajibu wa kuunga mkono kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel ICJ"
Jan 15, 2024 04:35Mwakilishi wa Slovenia katika Bunge la Ulaya amesema dunia ina jukumu la kuunga mkono kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya Israel, kutokana na jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Juhudi za utawala wa Kizayuni za kupotosha uhakika wa kutisha wa vita vya Gaza
Jan 13, 2024 08:46Kikao cha kusikiliza kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ, yenye makao yake huko Hague Uholanzi kimeanza katika hali ambayo mauaji ya kimbari na jinai za kivita za utawala wa Israel unaoiklia Quds kwa mabavu zingali zinaendelea katika ardhi za Palestina; na kila siku wananchi wa Palestina wanaendelea kuuliwa shahidi.
-
Kuanza kusikilizwa mashtaka ya Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki dhidi ya utawala wa Kizayuni
Jan 11, 2024 23:11Mahakama ya Kimataifa ya Haki yenye makao makuu yake mjini The Hague Uholanzi Alhamisi na Ijumaa inasikiliza na kukusanya mitazamo ya kisheria ya Afrika Kusini na utawala wa Kizayuni kuhusu kesi ya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza. Moja ya shughuli za mahakama hiyo ni kushughulikia mashtaka yanayohusiana na Mkataba wa Mauaji ya Kimbari wa 1948. Mkataba huo unatambuliwa rasmi na nchi 153.
-
Nchi za Kiarabu na Kiislamu zatakiwa kuunga mkono mashtaka ya Afrika Kusini dhidi ya Israel
Jan 03, 2024 03:40Gazeti moja la Misri limezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kuunga mkono mashtaka ya serikali ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki mjini The Hague.
-
Afrika Kusini yaushtaki utawala wa Kizayuni kwa kuendesha mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina
Dec 31, 2023 07:51Kufuatia kuendelea jinai za utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia, Afrika Kusini imeushtaki rasmi utawala huo katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki huko The Haque. Mastaka muhimu ya Afrika Kusini ni jinai za kivita, mauaji ya kizazi na kikabila huko Gaza na katika maeneo mengine ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ya Palestina.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran azungumza na waziri mwenzake wa Afrika Kusini, Ghaza maudhui kuu
Dec 20, 2023 23:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Afrika Kusini na kujadiliana naye masuala mbalimbali muhimu ya pande mbili, ya kieneo na ya kimataifa na hasa vita vya Ghaza huko Palestina.
-
Rais wa Afrika Kusini aitaka mahakama ya ICC ichunguze haraka jinai za kivita za Israel
Dec 19, 2023 23:58Rais wa Afrika Kusini ameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake huko Hague Uholanzi ichunguze haraka iwezekanavyo jinai za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ukanda wa Gaza.
-
Afrika Kusini yataka Israel itambulishwe kama "utawala wa kibaguzi"
Nov 25, 2023 01:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini ametangaza kwamba nchi hiyo inaendeleza juhudi katika mashirika na jumuiya za kimataifa za kuutambulisha utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni "utawala wa kibaguzi".