Afrika Kusini yataka Israel itambulishwe kama "utawala wa kibaguzi"
(last modified Sat, 25 Nov 2023 04:34:56 GMT )
Nov 25, 2023 04:34 UTC
  • Afrika Kusini yataka Israel itambulishwe kama

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini ametangaza kwamba nchi hiyo inaendeleza juhudi katika mashirika na jumuiya za kimataifa za kuutambulisha utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni "utawala wa kibaguzi".

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Naledi Pandor ameviambia vyombo vya habari kwamba: Afrika Kusini na Mamlaka ya Ndani ya Palestina zinafanyia kazi mikakati ya kiutendaji kwa ajili ya kuwasilisha kadhia ya Palestina kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ili mahakama hiyo iitambulishe Israel kama utawala wa ubaguzi wa rangi. 

Naledi Pandor

Kabla ya hapo, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini alikuwa ameiomba Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya The Hague kuchunguza jinai zilizofanywa na utawala wa Kizayuni wakati wa vita vya Gaza.

Jumanne iliyopita pia Bunge la Afrika Kusini lilipiga kura ya kufunga ubalozi wa utawala ghasibu wa Israel mjini Pretoria, kusimamisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala huo na kumfukuza balozi wa Israel nchini humo.

Itakumbukwa kuwa, maelfu ya Waafrika Kusini wamekuwa wakifanya maandamano ya kuiunga mkono Palestina na kulaani jinai za Israel hususan mauaji ya kimbari ya watoto wadogo na wanawake huko Gaza.

Maelfu ya watoto wa Gaza wameuawa katika mashambulizi ya Israel

Ofisi ya Habari ya Mamlaka ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imeangaza katika taarifa yake kwamba tangu tarehe 7 Oktoba, watu 14,854 wakiwemo watoto 6,150 na wanawake 4,000 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya Israel.

Tags