Pars Today
Jeshi la Somalia limefanikiwa kuua wanachama wasiopungua 30 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab katikati mwa nchi.
Jeshi la Somalia limetangaza kuwa, limeua wanamgambo 100 wa genge la kigaidi la al Shabab wakiwemo makamanda kadhaa wa genge hilo katika operesheni maalumu ya kijeshi huko kusini mwa Somalia.
Jeshi la Somalia limesema kuwa limeangamiza makumi ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab katika operesheni ya kiusalama kusini mwa Somalia.
Jeshi la Taifa la Somalia limetangaza kuwa, askari wa nchi hiyo wamefanikiwa kuzima mashambulio ya kundi la kigaidi la al-Shabaab yaliyolenga kambi mbili za kijeshi kusini mwa nchi.
Wizara ya Ulinzi ya Msumbiji imetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo limeanzisha oparesheni kubwa ya kukomboa mji wa pwani wa Palma unaodhibitiwa na kundi linalojiita al Shabab.
Wanamgambo wasiopungua 52 wa kundi la kigaidi la al-Shabaab wameangamizwa katika shambulio la wapiganaji hao dhidi ya jela moja iliyoko katika jimbo la Puntland,kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wanamgambo 15 wa kundi la kigaidi la al-Shabaab wameangamizwa katika operesheni ya jeshi la Somalia kusini mwa nchi.
Kwa akali watu watatu wameuawa huku wengine wengi wakijeruhiwa baada ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la al-Shabaab kushambulia hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu kwa mabomu na risasi.
Serikali ya Uganda imekadhibisha taarifa kuwa jeshi la nchi hiyo UPDF limeua wanachama 189 wa genge la al-Shabaab kusini magharibi mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Watu watano wameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa kwenye mlipuko uliojiri kwenye barabara ya mji wa Dhobley katika mkoa wa Lower Juba kusini mwa Somalia.