-
Bahrain, UAE zinakiuka haki za binadamu baada ya mgogoro na Qatar
Jun 15, 2017 03:22Umoja wa Mataifa umezitahadharisha nchi kadhaa za Ghuba ya Uajemi ambazo zinakiuka haki za binadamu kufuatia mgogoro ulioibuka na Qatar.
-
Kuendelea wasiwasi kuhusu hatima ya kiongozi wa Waislamu wa Kishia nchini Bahrain
Jun 12, 2017 03:31Takribani wiki tatu zimepita tangu askari wa utawala wa Aal Khalifa walipovamia nyumba ya Ayatullah Sheikh Isa Qassim, kiongozi wa Waislamu wa Kishia nchini Bahrain na kumwekea mzingiro wa nyumbani mwanazuoni huyo. Katika hali ambayo hakuna taarifa zozote hivi sasa kuhusu hatima ya Sheikh Isa Qassim, wananchi wa Bahrain pamoja na fikra za waliowengi hasa katika Ulimwengu wa Kiislamu wanafuatilia kwa wasiwasi habari mbalimbali kuhusu hali ya mambo nchini humo.
-
Safari ya pili ya Hamad bin Isa Aal Khalifa nchini Misri katika kipindi cha chini ya miezi mitatu
Jun 09, 2017 23:26Huku mivutano na mitibuano ya Waarabu kwa Waarabu katika eneo la Ghuba ya Uajemi ikiwa imezidi kupamba moto, Mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Aal Khalifa, ambaye siku tatu zilizopita alifanya safari ambayo haikuwa ya kushangaza mjini Riyadh, Saudi Arabia, baada ya kupita muda wa chini ya miezi mitatu, siku ya Alkhamisi alielekea tena Cairo mji mkuu wa Misri na tab'an jana Ijumaa alikuwa mgeni wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
-
Kituo cha Haki za Binadamu cha Bahrain chakosoa utendaji haribifu wa utawala wa Aal Khalifa
Jun 07, 2017 11:04Kituo cha Haki za Binadamu nchini Bahrain kimekosoa na kulaani utendaji wa utawala wa Kifalme wa nchi hiyo wa Aal Khalifa na kutoa wito wa kusitishwa utendaji huo haribifu.
-
Mfungamano mkubwa baina ya vitendo vya Aal Khalifa na utawala wa Kizayuni katika kukandamiza wapinzani
Jun 07, 2017 01:37Serikali ya ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain inafanya jinai kubwa dhidi ya raia wa kawaida, wanaharakati na shakhsia mbalimbali wa nchi hiyo kiasi kwamba vitendo vyake hivyo havina tofauti yoyote na jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.
-
Qatar: Madai dhidi yetu si ya kweli na hayana msingi
Jun 05, 2017 03:15Baada ya Saudi Arabia, Misri, Imarati na Bahrain kukata uhusiano na Qatar mapema leo Jumatatu, wizara ya mambo ya nje wa Qatar imesema, imesikitishwa na hatua hiyo.
-
Kuongezeka hasira za Wabahrain dhidi ya Marekani
Jun 02, 2017 21:58Habari kutoka nchini Bahrain zinaonesha kuongezeka mno hasira za wananchi wa nchi hiyo dhidi ya Marekani kutokana na siasa zake za kuunga mkono ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Aal Khalifa dhidi ya raia hususan kuendelea kuzingirwa nyumba ya Sheikh Isa Qassim kwa baraka kamili za Marekani.
-
Ghasia mpya Bahrain, Sheikh Qassim hajulikani aliko
May 29, 2017 02:41Askari wa utawala wa kiimla wa Bahrain wameendelea kuwashambulia wananchi wanaoandamana kumuunga mkono mwanazuoni wa Kiisalmu Sheikh Isa Qassim ambaye sasa ametoweka na hajulikani aliko.
-
Wasiwasi wa Umoja wa Ulaya kuhusiana na hali ya Bahrain
May 28, 2017 03:04Umoja wa Ulaya umetoa taarifa ambayo imeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya Bahrain na kutoa indhari kuhusiana na kuzidi kuwa mbaya hali ya nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.
-
Utawala wa Aal-Khalifa wapiga marufuku watu kushiriki mazishi ya watu uliowaua
May 27, 2017 09:07Utawala wa kidikteta wa Aal-Khalifa nchini Bahrain umepiga marufu kujitokeza watu katika mazishi ya mashahidi waliouawa na askari wa utawala huo eneo la Dizar, kaskazini magharibi mwa mkoa wa Pwani wa nchi hiyo.