Pars Today
Balozi wa Israel ametimuliwa nchini Colombia baada ya Bogota kuvunja uhusiano wake wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni kutokana na mashambulizi na jinai zisizokwisha za Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina hasa wa Ukanda wa Ghaza.
Saudi Arabia imetangaza kuteua balozi wake mpya nchini Syria ikiwa ni balozi wake wa kwanza baada ya zaidi ya muongo mmoja tangu ilipositisha uhusiano wake na serikali yar ais Bashar al-Assad.
Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa mashambulizi ya muungano wa nchi za Magharibi unaoongozwa na Marekani dhidi ya Yemen yamekiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa na hayana uhalali wowote.
Amir wa Qatar amemteua Sultan Salmeen Saeed Al-Mansouri kuwa balozi wa mpya wa nchi hiyo katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Serikali ya Iraq imemfukuza balozi wa Sweden mjini Baghdad kulalamikia serikali ya nchi hiyo ya Ulaya Magharibi ya kuruhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.
Baada ya Mali na Burkina Faso kuwafukuza mabalozi wa Ufaransa, majuzi Chad ilimpa balozi wa Ujerumani muda wa masaa 48 kuwa ameondoka nchini humo.
Wawakilishi wa Bunge la Jordan wamepigia kura ya ndio pendekezo la kufukuzwa balozi wa utawala haramu wa Israel huko Amman wakilalamikia na kupinga hatua ya waziri wa fedha katika serikali ya mrengo wa kulia ya Israel, ambaye alizua utata mapema wiki hii.
Waziri Mkuu wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen ameeleza kuwa, Uingereza si tu haiwezi kusaidia kupunguza mateso na masaibu ya kiuchumi ya wananchi wa Yemen bali nchi hiyo ni sehemu kuu ya njama ya kuvamiwa nchi hiyo.
Wananchi wa Lebanon wametoa mwito wa kutimuliwa nchini humo balozi wa Saudi Arabia wakimtuhumu kwamba, amekuwa akiingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.
Utawala haramu wa Israel umelazimika kumfuta kazi balozi wake wa nchini Morocco anayekabiliwa na kashfa za ngono na kuwanyanyasa kijinsia wanawake wa nchi hiyo ya Kiarabu.