-
Waislamu Canada wahofishwa na kuongezeka mashambulio ya chuki dhidi yao
Jun 15, 2021 03:52Waislamu nchini Canada wamesema kuwa wana wasiwasi na kuongezeka mashambulizi na vitendo vya chuki dhidi yao.
-
Maelfu waandamana kulaani 'Islamophobia' nchini Canada
Jun 12, 2021 13:10Maelfu ya watu wamefanya maandamano makubwa nchini Canada kulaani vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu, sambamba na kuonesha mshikamano wao na familia moja ya Kiislamu iliyouawa hivi karibuni katika mji wa London jimboni Ontario nchini humo.
-
Iran yalaani kitendo cha Canada kuzuia Wairani nchini humo kupiga kura uchaguzi wa rais
Jun 11, 2021 12:35Msemaji wa Tume ya Uchaguzi ya Iran amesema hatua ya Canada ya kukataa kutoa ushirikiano ili kuhakikisha Wairani wanaoishi Canada wanapiga kura katika uchaguzi wa rais wa Iran, ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa.
-
Mauaji ya familia ya Kiislamu nchini Canada, nembo ya Islamophobia katika nchi za Magharibi
Jun 09, 2021 11:30Kufuatia mauaji ya kikatili ya familia moja ya Kiislamu kwenye mji wa London katika jimbo la Ontario nchini Canada, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Justin Trudeau amesema anahidi kuwa, atachukua hatua zaidi za kukabiliana na makundi yenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia.
-
Baraza la Waislamu Canada lataka kukomeshwa chuki dhidi ya Uislamu nchini humo
Jun 08, 2021 18:46Baraza la Kitaifa la Waislamu wa Canada limetoa wito wa kutokomezwa haraka sera za chuki na kupiga vita Uislamu (Islamophobia) nchini humo baada ya jinai ya kutisha ya dereva mmoja kuwagonga watu watano wa familia moja na kuua wanne miongoni mwao.
-
Mwenye chuki dhidi ya Uislamu aua Waislamu 4 Canada kwa gari
Jun 08, 2021 08:11Dereva mmoja mwenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini Canada ameua watu wanne wa familia moja na kujeruhi mwingine vibaya, baada ya kuwagonga kwa makusudi na lori lake katika mkoa wa Ontario.
-
Wakazi asili wa Canada wakasirishwa na msimamo wa Papa Francis kuhusu maafa ya shule ya bweni ya Kamloops Indian
Jun 07, 2021 10:51Viongozi wa wakazi asili wa Canada na familia za wahanga wa shule za Kikatoliki nchini humo wameeleza kukasirishwa na matamshi na msimamo wa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani kuhusiana na maafa ya kaburi la umati la watoto 215 lililogunduliwa nchini Canada.
-
UN yataka kufanyike uchunguzi kuhusu kaburi la umati la watoto wa wakazi asilia wa Canada
Jun 05, 2021 07:19Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamezitaka Canada na Vatican kufanya uchunguzi kuhusu kaburi la umati lililogunduliwa likiwa na maiti 215 za watoto wa wakazi asilia katika jimbo la British Columbia huko Canada.
-
Vatican yashinikizwa kuomba radhi kwa kuhusika katika maafa ya wakazi asilia wa Canada
May 30, 2021 10:42Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, kufuatia kugunduliwa mabaki ya maiti za watoto 215 wa wakazi asilia wa Canada katika eneo la shule ya zamani ya bweni ya kanisa Katoliki huko magharibi mwa nchi hiyo, miito ya kulitaka kanisa hilo liombe radhi kutokana na maafa ya watoto hao imeongezeka zaidi.
-
Canada: Kundi la wafuasi wa Trump wenye misimamo ya kufurutu ada ni la kigaidi
Feb 04, 2021 07:41Canada imeliweka katika orodha yake ya makundi ya kigaidi kundi la mrengo wa kulia lenye misimamo ya kuchupa mipaka kwa jina la "Proud Boys" ambao ni wafuasi nambari moja wa Trump. Kundi hilo la wafuasi wa Trump wamewekwa na Canada katika orodha yake ya makundi ya kigaidi pamoja na makundi ya al Qaida na Daesh.