-
Rais Samia awatahadharisha Watanzania dhidi ya Corona
Jun 02, 2021 04:25Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania waendelee kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.
-
WHO: Corona haitamalizika kabla ya asilimia 70 ya walimwengu kupewa chanjo
May 29, 2021 07:08Mkurugenzi wa Shirika la Afya Dunia (WHO) kanda ya Ulaya amesema kuwa maambukizi ya virusi vya corona hayawezi kukomeshwa hadi pale asilimia 70 ya watu wote duniani watakapopata chanjo ya kukabiliana na virusi hivyo.
-
Indhari ya Shirika la Afya Duniani kuhusu 'apartheid (ubaguzi) ya chanjo'
May 18, 2021 10:08Katika hali ambayo, maradhi ya Covid-19 yameendelea kuua watu katika pembe mbalimbali za duniani, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameashiria hali ya kusikitisha ya usambazaji chanjo ya kukabiliana na virusi vya corona na kusema kwamba, kwa bahati mbaya ulimwengu umeingia katika hatua ya 'apartheid (ubaguzi) ya chanjo.'
-
Maiti za wagonjwa wa corona zatoswa kwenye Mto Ganga nchini India
May 11, 2021 13:10Baadhi ya vyombo vya habari vya India vimeripoti kuwa viwiliwili vya watu waliofariki kwa ugonjwa wa Covid-19 nchini humo vimeonekana vikielea kwenye Mto mkubwa wa Ganga wa nchi hiyo.
-
Afrika Kusini yasema nchi tajiri zinafanya 'apartheid ya chanjo' ya Corona
May 11, 2021 02:50Rais wa Afrika Kusini ametahadharisha kuwa, iwapo nchi tajiri duniani zitaendelea kuhodhi chanjo za ugonjwa wa Covid-19, huku mamilioni ya watu katika nchi masikini wakiendelea kuaga dunia kwa kukosa chanjo hizo, kitendo hicho ni sawa na 'apartheid ya chanjo.'
-
Misikiti India yageuzwa kuwa vituo vya wagonjwa wa Covid-19
May 11, 2021 02:50Aghalabu ya misikiti nchini India imegeuzwa na kuwa vituo vya kuwapokea wagonjwa wa Covid-19, huku mfumo wa afya wa nchi hiyo ukiendelea kulemewa kupita kiasi, vitanda kufurika mahospitalini, sambamba na kushuhudia uhaba mkubwa wa dawa na hewa ya oksijeni katika wimbi la pili la Corona nchini humo.
-
Corona imeua watu karibu milioni 7 duniani, maradufu ya idadi iliyotangazwa
May 07, 2021 07:43Taasisi moja ya kutathmini data za afya katika Chuo Kikuu cha Washington DC nchini Marekani imesema idadi ya watu walioaga dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19 duniani ni mara mbili ya idadi iliyotangazwa kufikia sasa.
-
Taifa lililochanja idadi kubwa zaidi ya jamii yake larejesha sheria za kudhibiti Corona
May 05, 2021 07:02Kisiwa cha Ushelisheli ambacho kimewapiga chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 asilimia 60 ya jamii yake kimerejesha tena sheria za kudhibiti msambao wa virusi vya Corona, baada ya kesi ya maambukizi kuongezeka kwa kiwango cha kutisha nchini humo.
-
Tathmini ya siku 100 za serikali ya Biden kuwa ofisini
May 02, 2021 02:22Baada ya kupita siku 100 tokea Rais Joe Biden wa chama cha Democrat achukue madaraka ya Marekani, watu wamekuwa wakitathmini utendaji wa serikali yake katika kipindi hiki, kipindi ambacho baadhi ya wataalamu wanasema kwamba licha ya kufanikiwa katika baadhi ya sehemu lakini ameshindwa pakubwa kutekeleza ahadi alizotoa katika kampeni za uchaguzi.
-
Moto waua 18 katika hospitali ya wagonjwa wa Corona India
May 01, 2021 12:49Kwa akali watu 18 wamepoteza maisha katika ajali ya moto iliyotokea katika hospitali moja ya wagonjwa wa Corona nchini India, huku nchi hiyo ya Asia leo Jumamosi ikiweka rekodi mpya ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.