-
Abubakr al-Baghdadi, kiongozi wa Daesh auawa
Oct 27, 2019 04:08Afisa mmoja wa Pentagon nchini Marekani amesema kuwa Abubakr al-Baghdadi, kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh ameuawa katika operesheni ya siri iliyotekelezwa kaskazini magharibi mwa Syria.
-
Mauaji ya kigaidi yaongezeka Iraq baada ya Marekani kuwahamishia nchini humo magaidi wa ISIS
Oct 25, 2019 03:42Mauaji ya kigaidi yameongezeka dhidi ya maafisa wa serikali ya Iraq baada ya Marekani kuwahamishia nchini humo magaidi wa Daesh (ISIS) kutoka kaskazini mwa Syria kufuatia kushadidi mashambulizi ya Uturuki huko Syria.
-
Trump na misimamo ya undumakuwili kuhusu magaidi wa Daesh (ISIS)
Oct 15, 2019 04:40Licha ya Rais Donald Trump wa Marekani kutoa onyo kuhusiana na kuibukka upya shughuli za kundi la kigaidi la Daesh (ISIS), kitendo cha kuondoa askari wa Kimarekani katika maeneo yanayoshambuliwa na Uturuki huko kaskazini mwa Syria, kimeandaa uwanja wa kufufuka upya kundi hilo la ukufurishaji ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Indhari kuhusu kujiunga viongozi wa Taliban na kundi la Daesh huko Afghanistan
Oct 06, 2019 04:31Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Afghanistan ametahadharisha kuhusu kujiunga viongozi wa kundi la Taliban na kundi la kigaidi la Daesh nchini humo.
-
DAESH (ISIS) laua askari 14 katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria
Sep 26, 2019 04:05Kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS) limetangaza kuwa, limewaua askari 14 wa jeshi la Nigeria katika shambulio lililofanya hapo jana katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
-
Trump azionya nchi za Ulaya, azitaka ziwachukue raia wake waliojiunga na ISIS
Sep 21, 2019 07:45Rais Donald Trump wa Marekani amezionya nchi za Ulaya akizitaka zihakikishe zimewachukua raia wao waliojiunga na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) na wanaoendelea kushikiliwa nchini Iraq na Syria.
-
Maiti za zaidi ya wahanga elfu 12 wa Daesh zagunduliwa katika makaburi ya umati, Iraq
Aug 31, 2019 22:12Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu nchini Iraq imetangaza kuwa, maiti elfu 12 za wahanga wa ukatili na jinai za kundi la kigaidi la Daesh zimegunduliwa katika zaidi ya makaburi 200 ya umati.
-
Tishio jingine la Donald Trump la kuwahamishia magaidi wa Daesh katika nchi za Ulaya
Aug 22, 2019 21:55Nafasi ya Marekani na washirika wake wa Magharibi na wa Kiarabu katika kuanzisha na kueneza harakati za makundi ya kigaidi na kitakfiri likiwemo la Daesh si ya kukanushika hata kidogo.
-
Umoja wa Mataifa walaani shambulio la kigaidi Kabul, Afghanistan
Aug 19, 2019 03:45Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali shambulio la kigaidi la Kabul, mji mkuu wa Afghanistan lililosababisha makumi ya watu kuuawa na kulitaja kuwa linatisha.
-
London yakataa kuwapokea watoto wa magaidi wa Daesh raia wa Uingereza
Aug 13, 2019 22:04Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa watoto wa magaidi wa wanamgambo wa Daesh raia wa nchi hiyo ambao wako katika maeneo yaliyokumbwa na vita hawatarejeshwa nchini.