Umoja wa Mataifa walaani shambulio la kigaidi Kabul, Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i55469-umoja_wa_mataifa_walaani_shambulio_la_kigaidi_kabul_afghanistan
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali shambulio la kigaidi la Kabul, mji mkuu wa Afghanistan lililosababisha makumi ya watu kuuawa na kulitaja kuwa linatisha.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 19, 2019 03:45 UTC
  • Umoja wa Mataifa walaani shambulio la kigaidi Kabul, Afghanistan

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali shambulio la kigaidi la Kabul, mji mkuu wa Afghanistan lililosababisha makumi ya watu kuuawa na kulitaja kuwa linatisha.

Stéphane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Antonio Guterres ametoa taarifa na kuonyesha masikitiko yake sambamba na kutangaza kuwa pamoja na familia za wahanga wa shambulio hilo la kigaidi.

Aidha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, umoja huo uko pamoja na serikali na wananchi wa Afghanistan katika kipindi hiki cha msiba na maombolezo.

Watu 63 waliouawa katika shambulio la kigaidi lililotokea juzi mjini Kabul, Afghanistan na makumi ya wengine wakijeruhiwa.

Stéphane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan imetangaza kuwa, shambulio hilo la bomu lililenga hafla ya harusi katika wilaya ya 6 mjini Kabul. 

Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuwa, ndilo lililotekeleza shambulio hilo.

Katika miezi ya hivi karibuni maeneo mbalimbali ya mji mkuu wa Afghanistan, Kabul yameshuhudia ongezeko la mshambulizi ya kigaidi. Kundi la kigaidi la Daesh na lile la Taliban yametangaza kuhusika na mengi kati ya mashambulio hayo ambayo yameua makumi ya raia wasio na hatia. 

Mashambulizi ya kigaidi yameshadidi nchini Afghanistan licha ya Marekani na waitifaki wake kutuma majeshi nchini humo tangu mwaka 2001 kwa kile kilichosemwa ni kwenda kupambana na ugaidi na kurejesha amani nchini Afghanistan.