London yakataa kuwapokea watoto wa magaidi wa Daesh raia wa Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i55363-london_yakataa_kuwapokea_watoto_wa_magaidi_wa_daesh_raia_wa_uingereza
Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa watoto wa magaidi wa wanamgambo wa Daesh raia wa nchi hiyo ambao wako katika maeneo yaliyokumbwa na vita hawatarejeshwa nchini.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 14, 2019 02:34 UTC
  • London yakataa kuwapokea watoto wa magaidi wa Daesh raia wa Uingereza

Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa watoto wa magaidi wa wanamgambo wa Daesh raia wa nchi hiyo ambao wako katika maeneo yaliyokumbwa na vita hawatarejeshwa nchini.

Ikifafanua sababu ya kuchukua uamuzi huo, serikali ya Uingereza imesema kuwa kuwatuma wanajeshi katika kambi Syria kwa ajili ya kuwanusuru watoto hao ni jambo la hatari sana. Hiyo ni moja ya hatua za mwisho alizozichukua Sajid Javid alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza. Aidha kuna wasiwasi kwamba wazazi wa watoto hao ambao wamefutiwa haki yao ya uraia wanaweza kuwatumia watoto wao hao ili kurejeshewa haki yao ya uraia. 

Sajid Javid

Kuna uwezekano pia kwamba uamuzi huo wa Sajid Javid, Waziri Mpya wa Fedha wa Uingereza utakosolewa pakubwa na taasisi za kuwatetea watoto na makundi ya kibinadamu yanayowasaidia watoto huko Syria. Hii ni kwa sababu makundi hayo yanaamini kuwa watoto wasio na hatia hawapasi kutwishwa makosa ya wazazi wao. Kundi la kigaidi la Daesh limekuwa likiwatumia watoto wakati wa kuanda video zao za propaganda na oparesheni za kigaidi. 

Huko nyuma pia, Berlin ilitangaza kuhusu kurejea kutoka Syria raia wa Ujerumani wanachama wa Daesh ikisema kuwa jambo hilo litatekelezwa haraka iwezekanavyo baada ya kutiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani watu hao.