Nov 07, 2023 02:31
Mwezi mmoja ukiwa umepita tangu kujiri operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na utawala wa Kizayuni kuanzisha mashambulizi makali ya mabomu ambayo hajawahi kushuhudiwa tena huko Ghaza, ambayo yamepelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa makumi ya maelfu ya Wapalestina, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake, mwenendo wa upinzani dhidi ya vitendo hivyo vya jinai vya Israeli, umeongezeka sana duniani ikiwa ni pamoja na nchini Marekani, ambayo ni mwitifaki mkubwa wa Tel Aviv.