HAMAS: Muqawama wa watu wa Gaza umeipigisha magoti Israel
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, kusimama kidete watu wa Gaza na vikosi vya muqawama kumeshinda lengo la utawala unaokalia kwa mabavu la kuwatimua Wapalestina.
Hazem Qassem", msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), ameongeza kuwa kurejea wakimbizi wa Kipalestina kaskazini mwa Ukanda wa Gaza baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano, ambayo yalitarajiwa, kunaonyesha kushindwa kwa moja ya malengo ya vita Ukanda wa Gaza ya kuwafukuza watu wa ardhi ya Palestina.
Afisa huyo wa HAMAS amesisitiza kuwa, kusimama kidete wananchi wa Gaza kumeipigisha magoti Israel na kuilazimisha ikubali kusitisha vita na mauaji yake ya kinyama katika Ukanda wa Gaza.
Msemaji huyo wa harakati ya Hamas amesisitiza kuwa, mizizi ya wananchi wa Palestina licha ya kuwepo vita vya mauaji ya halaiki ambayo haijawahi kushuhudiwa, ilisababisha vita vya kuwepo Wapalestina katika ardhi hii kwa ajili ya kuwapendelea wananchi wa Palestina.
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema bayana kwamba, hakuna nguvu inayoweza kuharibu azma ya wananchi wa Palestina ya kuelekea katika ukombozi na mamlakka yao ya kujitawala.
Jumatano, Januari 15, 2025, Serikali ya Qatar ilitangaza kupatikana mafanikio ya juhudi za kusimamisha mapigano katika Ukanda wa Ghaza kati ya pande za Palestina na Israel, na utekelezaji wa makubaliano hayo ulianza kutekelezwa Jumapili, Januari 19 na hivyo kuhitimisha miezi zaidi ya15 ya vita vya kinyama na mauaji ya kimbari ya zaidi ya watu 46,000 yaliyofanywa na jeshi la Kizayuni.