Hamas: Wananchi wa Palestina watabaki katika ardhi yao
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121962-hamas_wananchi_wa_palestina_watabaki_katika_ardhi_yao
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa wananchi wa Palestina wako imara katika ardhi yao na mpango wowote wa kuwahamisha utafeli. Amesisitiza kuwa: Wapalestina watabaki katika ardhi yao.
(last modified 2025-01-27T07:21:27+00:00 )
Jan 27, 2025 07:21 UTC
  • Hamas: Wananchi wa Palestina watabaki katika ardhi yao

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa wananchi wa Palestina wako imara katika ardhi yao na mpango wowote wa kuwahamisha utafeli. Amesisitiza kuwa: Wapalestina watabaki katika ardhi yao.

Abdul Latif al Qanou ameeleza kuwa kile ambacho maghasibu wa Israel hawakuweza kukipata kutoka kwa wananchi wa Palestina kupitia vita hawatakipata kupitia njama za kuwafukuza raia hao katika ardhi yao na kuwafanya wakimbizi.

Msemaji wa Hamas ameongeza kuwa utawala wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu unafanya kila uwezalo kukiuka majukumu yake kwa mujibu wa makubaliano ya kusitisha vita, hata hivyo hawataruhusu hilo lifanyike. 

Huko nyuma pia Hazim Qassim msemaji mwingine wa Hamas alisisitiza kuwa kurejea nyumbani wakazi wa kaskazini mwa Gaza ni ishara ya kushindwa adui kuwafurusha Wapalestina katika ardhi yao. 

Amesema hakuna nchi yoyote inayoweza kusitisha harakati ya wananchi wa Palestina ya kupigania uhuru wao na kujitawala.