Ripoti: Wazayuni wanawatesa mateka wa Kipalestina kabla ya kuwaachia huru
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i122214-ripoti_wazayuni_wanawatesa_mateka_wa_kipalestina_kabla_ya_kuwaachia_huru
Baada ya kumalizika awamu ya nne ya kubadilishana mateka kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Muqawama wa Palestina, duru za habari zimearifu kuwa baadhi ya mateka wa Kipalestina wamejeruhiwa kutokana na kuteswa kabla ya kuachiwa huru.
(last modified 2025-02-02T07:42:15+00:00 )
Feb 02, 2025 07:42 UTC
  • Ripoti: Wazayuni wanawatesa mateka wa Kipalestina kabla ya kuwaachia huru

Baada ya kumalizika awamu ya nne ya kubadilishana mateka kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Muqawama wa Palestina, duru za habari zimearifu kuwa baadhi ya mateka wa Kipalestina wamejeruhiwa kutokana na kuteswa kabla ya kuachiwa huru.

Vyombo vya habari vya Palestina vimetangaza kuwa, baadhi ya mateka walioachiwa huru waliteswa na walinzi wa magereza ya Israel kwa siku kadhaa kabla ya kuachiwa huru na sasa wamepelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu kutokana na majeraha na madhara mengi waliyoyapata.

Klabu ya Mateka kwa Kipalestina imetangaza kuhusiana na kadhia hii kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya ugaidi ulioratibiwa dhidi ya mateka wa Kipalestina iliowaachia huru na umezikataza familia za mateka hao kuwaandalia mapokezi ya aina yoyote. 

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) pia imesisitiza katika taarifa yake kuwa, unyanyasaji wa kutisha na unaoendelea magerezani dhidi ya mateka hao mashujaa ni jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu na kuna ulazima Umoja wa Mataifa na taasisi za haki za binadamu kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ili kukomesha vitendo hivyo vya Wazayuni na kuwawajibisha wahusika.