Pars Today
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, matamshi Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina katu hayaakisi msimamo wa wananchi wa taifa hilo madhulumu.
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas amesisitiza kuwa wananchi wa Palestina wataendelea kufanya maandamano makubwa ya "Haki ya Kurejea" hadi pale malengo yao yatakapofanikishwa na kuvunjwa mzingiro wa Ghaza.
Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesisitiza kuwa, harakati hiyo haiko tayari kulipa gharama yoyote ile ya kisiasa mkabala na kuondolewa mzingiro wa utawala ghasibu wa Israel wa zaidi ya miaka 12 dhidi ya Ukanda wa wa Gaza.
Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema shambulio la ndege za kivita za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza dhidi ya kituo cha brigedi za Izzuddin al-Qassam, tawi la kijeshi la harakati hiyo ambalo limesababisha kuuawa shahidi wanamapambano wawili wa Muqawama halitaachwa bila kujibiwa.
Mjumbe wa kamati kuu ambaye pia ni mkuu wa kamati ya ufuatiliaji maridhiano ya kitaifa wa harakati ya Fat-h amesema harakati hiyo imetoa jibu chanya la maandishi kwa maafisa wa Misri kuhusiana na mapendekezo yaliyowasilishwa na nchi hiyo kuhusu maridhiano ya kitaifa ya Palestina.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imeuonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel, kutokana na hatua yake ya kuzidisha mzingiro katika Ukanda wa Gaza.
Balozi wa Qatar huko Palestina amesema kuwa utawala wa Kizayuni unapasa kukubali matakwa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) kuhusu eneo la Ukanda wa Ghaza kwa sababu harakati hiyo sasa iko imara zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma.
Mjumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amekanusha vikali baadhi ya madai kuhusiana na kukubali kujadili viongozi wa harakati hiyo mpango wa "Muamala wa Karne".
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, HAMAS, imesisitiza kuwa, jukumu la kutetea haki zote za kisiasa na kifedha za wakimbizi Wapalestina ni la jamii ya kimataifa na hasa Umoja wa Mataifa.
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupasisha azimio linaloulaumu na kuulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kufanya mauaji dhidi raia wa Kipalestina katika Ukanda wa Ghaza ni ithibati nyingine inayoonesha namna na utawala huo haramu na Marekani zinazidi kutengwa kimataifa.