-
Hamas: US ni mshiriki wa jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza
Aug 28, 2025 22:54Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema hatua ya Marekani ya kutumia turufu dhidi maazimio ya Umoja wa Mataifa "inaifanya kuwa mshiriki" wa jinai za utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Hamas yakadhibisha madai ya kuuawa kigaidi Khalil al-Hayya
Aug 27, 2025 06:52Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imepinga madai ya utawala haramu wa Israel kwamba umemuua kigaidi Khalil al-Hayya, mmoja wa viongozi waandamizi wa kundi hilo la Muqawama.
-
Hamas, Jihadul Islami zalaani uvamizi wa kifashisti wa Israel dhidi ya Yemen
Aug 25, 2025 07:14Harakati za Muqawama wa Kiislamu za Palestina za Hamas na Jihadul Islami zimeshutumu vikali mashambulizi mabaya ya Israel dhidi ya mji mkuu wa Yemen na miundombinu ya kiraia, na kuyaelezea kama "ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa" na gharama ya kuilinda Palestina.
-
Ufaransa 'yamjia juu' balozi wa US Paris kwa kuituhumu kuwa inahatarisha maisha ya Mayahudi
Aug 25, 2025 03:08Ufaransa imemwita balozi wa Marekani nchini humo Charles Kushner, baada ya mwanadiplomasia huyo kumwandikia barua Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akidai kwamba Paris imeshindwa kuchukua hatua za kutosha kukomesha vitendo vya mabavu dhidi ya Mayahudi raia wa nchi hiyo.
-
Hamas yapongeza 'ujasiri' wa mawaziri wa Uholanzi kujiuzulu juu ya Gaza
Aug 24, 2025 23:27Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imepongeza hatua ya kujiuzulu mawaziri kadhaa wa Uholanzi, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Caspar Veldkamp, kujibu hatua ya kukataa kwa serikali yao kuiwekea vikwazo Israel. Hamas imetaja kujiuzulu huko kama uamuzi wa kijasiri na wa kimaadili.
-
Hamas yaonya: Israel haitafikia malengo yake Ukanda wa Gaza
Aug 21, 2025 03:01Utawala wa Israel umeanza kupeleka vikosi vya jeshi lake kwenye viunga vya Jiji la Gaza kwa ajili ya kuanza kutekeleza mpango wake wa kukalia kwa mabavu eneo hilo kubwa zaidi la Ukanda wa Gaza, lakini Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeonya kuwa, Tel Aviv itashindwa kutimiza malengo yake.
-
Hamas yapasisha pendekezo la Qatar na Misri la kuhitimisha vita vya Israel dhidi ya Gaza
Aug 19, 2025 08:06Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imesema kuwa imepasisha pendekezo jipya la Qatar na Misri la kuhitimisha vita vya mauaji ya kimbari vya Israel katika Ukanda wa Gaza
-
Hamas: Israel imeingia katika marhala mpya ya mauaji ya kimbari Gaza
Aug 17, 2025 23:57Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imelaani vikali mpango wa Israel wa kukalia kwa mabavu Jiji la Gaza na kuwahamisha kwa nguvu wakazi wake na kusisitiza kuwa, huo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
-
HAMAS: Mpango wa Netanyahu wa 'Israel Kubwa Zaidi' ni tishio la wazi kwa mataifa ya Kiarabu na Waislamu
Aug 15, 2025 04:00Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS ametahadharisha kuhusu kupanuliwa kwa mipango ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kueleza kwamba hatua hiyo inakwenda sambamba na matamshi na ndoto za Benjamin Netanyahu kuhusu kuasisi "Israel Kubwa Zaidi."
-
Netanyahu na genge lake wapitisha mpango wa kuikalia Ghaza City, Hamas yatoa mjibizo mkali
Aug 08, 2025 07:55Liitwalo 'baraza la mawaziri la kisiasa na kiusalama' la utawala haramu wa kizayuni wa Israel limeidhinisha mpango wa waziri mkuu wa utawala huo ghasibu Benjamin Netanyahu wa kulikalia kwa mabavu eneo lote la Ukanda wa Ghaza kwa kuwahamisha kwanza kwa nguvu makumi ya maelfu ya Wapalestina wa Ghaza City.