-
Hizbullah: Israel 'itafutwa' ikiwafukuza Wapalestina Gaza
Nov 16, 2023 02:58Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala haramu wa Israel utasambaratishwa na kufutwa katika uso wa dunia iwapo utajaribu kuwafurusha wananchi wa Palestina wanaoshi katika Ukanda wa Gaza.
-
Israel yafyata mkia, yasema haitaki kuingia vitani na Hizbullah
Oct 25, 2023 04:06Rais Isaac Herzog wa Israel amedai kuwa, utawala huo wa Kizayuni hauna azma ya kuingia vitani na Harakati ya Hizbullah ya nchini Lebanon katika upande wa kaskazini, siku chache baada ya viongozi wa Marekani kuwatahadharisha watawala wa Israel kuhusu ugumu na hatari ya kuendesha vita viwili kwa wakati mmoja; upande wa kusini na Harakati ya Hamas ya Palestina na upande wa kaskazini na harakati yenye nguvu kubwa ya kijeshi, Hizbullah.
-
Hizbullah yatoa taarifa kuhusu mashambulio makali iliyofanya dhidi ya ngome za Israel
Oct 14, 2023 23:03Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa na kutangaza kuwa imetoa kipigo kikali katika mashambulio iliyofanya dhidi ya ngombe za jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika katika mashamba ya Shabaa ya ardhi ya Lebanon inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
-
Afisa wa usalama wa utawala wa Israel: Maneno ya Nasrullah hayapaswi kupuuzwa
Aug 19, 2023 22:57Naibu Mkuu wa Shirika la Usalama la utawala wa Kizayuni wa Israel amesema kwamba, matamshi yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah, hayapaswi kupuuzwa.
-
Hizbullah: Hakuna njia ya kujitoa katika mzozo wa urais isipokuwa mazungumzo
Jun 27, 2023 01:06Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria mgogoro kuhusu suala la kumchagua rais mpya wa nchi hiyo na kusema mazungumzo ndiyo njia pekee ya kuondokana na mgogoro huo. Amesisitiza kuwa kuendelea hitilafu juu ya suala hilo hakuna manufaa yoyote.
-
"Njia za chini ya ardhi za Hizbullah"; zilzala haribifu kwa utawala wa Kizayuni
Jun 18, 2023 00:54Duru za habari za lugha ya Kiibrania zimetangaza kuwa Harakati ya Mapambano ya Lebanon ya Hizbullah inaimarisha nguvu na uwezo wake wa chini ya ardhi na kwamba harakati hiyo inaweza kubomoa na kuharibu vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kupitia njia hizo za nchini ya ardhi.
-
Sheikh Naim Qassim: Makubaliano ya Iran na Saudi Arabia yalikuwa ya kishujaa
Apr 20, 2023 03:24Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni baina ya Iran na Saudi Arabia ya kuanzisha tena uhusiano wao wa kidiplomasia yalikuwa ya kishujaa.
-
Hezbollah ya Lebanon yatahadharisha kuhusu kuchelewa kuanzisha uhusiano na Syria na China
Apr 17, 2023 21:58Mwakilishi wa Baraza Kuu la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa hii leo Ulimwengu wa Kiarabu unaelekea upande wa Syria kwa uamuzi wake na kwa kuzingatia maslahi yake.
-
Maafisa wa Iran, Lebanon wazungumzia matukio ya kieneo mjini Beirut
Mar 24, 2023 04:21Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Mahusiano ya Kigeni la Iran, Kamal Kharrazi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah mjini Beirut, ambapo wamejadili matukio ya hivi sasa ya kisiasa na kiusalama katika eneo la Asia Magharibi.
-
Hizbullah: Tupo tayari kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Syria
Feb 10, 2023 03:27Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa ikisisitiza uungaji mkono wa pande zote wa muqawama wa Lebanon kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi huko Syria na kusisitiza kuwa itatumia suhula zake zote kuisaidia na kuihudumia serikali na wananchi wa Syria katika mazingira haya magumu baada ya zilzala.