Hizbullah: Tupo tayari kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i93884-hizbullah_tupo_tayari_kuwasaidia_waathirika_wa_tetemeko_la_ardhi_syria
Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa ikisisitiza uungaji mkono wa pande zote wa muqawama wa Lebanon kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi huko Syria na kusisitiza kuwa itatumia suhula zake zote kuisaidia na kuihudumia serikali na wananchi wa Syria katika mazingira haya magumu baada ya zilzala.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 10, 2023 03:27 UTC
  • Hizbullah: Tupo tayari kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Syria

Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa ikisisitiza uungaji mkono wa pande zote wa muqawama wa Lebanon kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi huko Syria na kusisitiza kuwa itatumia suhula zake zote kuisaidia na kuihudumia serikali na wananchi wa Syria katika mazingira haya magumu baada ya zilzala.

Tetemeko la ardhi lililokuwa na ukubwa wa 7.8 kwa kipimo cha rishta lilitokea asubuhi ya Jumatatu wiki hii kusini mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria; ambapo kwa mujibu wa takwimu za karibuni hadi sasa watu 2,902 wameaga dunia na 5,085 wamejeruhiwa kufuatai tetemeko hilo huko Syria.  syria

Tetemeko la ardhi Syria 

Televisheni ya al Aalam ya Iran imeripoti kuwa, harakati ya Hizbullah ya Lebanon jana usiku ilitangaza kuwa itastafidi na suhula na uwezo wake wote kuihudumia serikai na watu wa Syria na kwamba haijawahi kusita kuwaunga mkono wananchi wa Syria. 

Taarifa ya Hizbullah ya Lebanon imeongeza kuwa, tunataka kushirika pakubwa katika kampeni ya masuala ya kibinadamu na yoyote atakayependa kutoa msaada afike katika vituo vya misaada na huduma za mji katika Shirika la Afya la Lebanon. 

Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon Jumanne wiki hii pia ilitoa taarifa ikitoa mkono wa pole kwa wananchi wa Uturuki na Syria na kuzitolea wito nchi zote na taasisi za kimataifa kutumia suhula zote zilizopo kuzisaidia nchi mbili hizo zilizoathiriwa na tetemeko la ardhi.