-
Ayatullah Khatami: Adui atakumbwa na usiku wa giza iwapo atasababisha madhara kwa Iran
Dec 26, 2025 12:07Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesisitiza kuwa, uwezo wa makombora wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utaendelea kuwepo na kwamba: "Maadui watakumbana na usiku wa giza kama wanataka kuidhuru Jamhuri ya Kiislamu.
-
Gharibabadi: Mashambulizi ya adui dhidi ya raia wakati wa vita yamethibitisha suala la nyuklia lilikuwa kisingizio tu
Dec 26, 2025 11:55Kazem Gharibabadi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisheria na Kimataifa ameissitiza kuwa mashambulizi ya adui dhidi ya raia na makazi ya watu wakati wa vita haramu vilivyoanzisha na Israel kwa kushrikiana na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwezi Juni mwaka huu yamethibitisha kuwa kadhia ya nyuklia ilikuwa kisingiizo tu cha kuishambulia nchi hii.
-
Shukurani za Venezuela kwa Iran kwa msimamo wake thabiti wa kuitetea Caracas
Dec 26, 2025 02:48Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Venezuela ameisifu Iran kwa misimamo yake thabiti ya kutetea mamlaka ya kujitawala Caracas.
-
IRGC yanasa meli iliyobeba lita milioni 4 za mafuta ya magendo
Dec 25, 2025 07:18Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limekamata meli iliyokuwa imebeba shehena kubwa ya mafuta ya magendo katika maji ya Ghuba ya Uajemi.
-
Iran yasuta 'diplomasia ya mabomu' ya Marekani
Dec 25, 2025 06:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amekejeli na kukosoa vikali tafsiri ya Marekani ya 'diplomasia' katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, akisisitiza kuwa, uwazi na utayarifu kwa mazungumzo hauna mfungamano wowote na kuuripua kwa mabomu upande wa pili wakati wa majadiliano.
-
UWW: Muirani Amouzad ndiye mwanamieleka 'Aliyetamalaki Zaidi' duniani 2025
Dec 25, 2025 05:42Muungano wa Mieleka Duniani (UWW) umemtaja Rahman Amouzad kutoka Iran kuwa mwanamieleka wa mtindo wa freestyle (kujiachia) "Aliyeng'ara Zaidi" kwa mwaka huu 2025.
-
Utayari wa Iran wa kuanzisha mtandao wa nchi za Kiislamu wa bioteknolojia na kuimarisha usalama wa chakula
Dec 24, 2025 08:34Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Bioteknolojia ya Kilimo ya Iran ametangaza utayari wa kuanzisha mtandao wa pamoja wa ushirikiano wa kisayansi na utafiti na nchi za Kiislamu katika sekta ya usalama wa chakula.
-
Mwakilishi wa Iran UN: Baada ya Oktoba 2025, Azimio 2231 halikuwa tena na itibari ya kisheria
Dec 24, 2025 06:47Mwakilishi wa Iran katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa cha kujadili Azimio 2231 amesema, Jamhuri ya Kiislamu inakubaliana na misimamo ya Russia na China ya kupinga kuitishwa kwa kikao hicho. Azimio 2231 lina kifungu kinachoeleza bayana kwamba muda wake wa kumalizika ni Oktoba 2025, na baada ya hapo hakutakuwa tena na msingi wa kisheria wa kuendelea majukumu ya azimio hilo.
-
"Uwezo wa makombora ya Iran umeimarika, tayari kukabili adui"
Dec 24, 2025 02:40Msemaji wa Jeshi la Iran amesema kwamba, uwezo wa vikosi vya majini, ardhini, na makombora vya Jamhuri ya Kiislamu viko tayari kikamilifu kukabiliana na senario yoyote tarajiwa ya adui, akisisitiza kwamba Tehran bado haijatumia nguvu yake halisi ya makombora.
-
Rais Pezeshkian awasilisha rasimu ya bajeti katika Bunge la Iran
Dec 23, 2025 13:33Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amewasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka ujao wa kifedha wa Iran (kuanzia Machi 21, 2026) katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran).