-
"Mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza yanakanyaga sheria za kimataifa"
Nov 13, 2023 23:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran sajari na kulaani mauaji ya halaiki ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza amesisitiza kuwa, jinai zinazofanywa na Wazayuni katika eneo hilo lililozingira ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
-
SEPAH: Jinai za Wazayuni haziwezi kuzuia ushindi wa Wapalestina; Iran imejiandaa kwa hali zote
Nov 13, 2023 23:05Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, kamwe jinai za utawala wa Kizayuni haziwezi kuzuia ushindi wa Wapalestina, na pia Marekani itambuwe kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ina nguvu kubwa na hakuna mtu anayeweza kuliteteresha taifa la Iran kwa vitisho vyake.
-
Aban 13, Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari wa Kimataifa
Nov 13, 2023 08:21Assalamu alaykum wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran popote pale mlipo hasa huko nyumbani Afrika Mashariki. Ni matumaini yangu kuwa, mubukheir wa afya na mnaendelea vyema katika kutekeleza majukumu yenu ya kila siku.
-
Iran na China zakubaliana kuanzisha kituo cha pamoja cha mafunzo ya teknolojia mpya
Nov 11, 2023 23:26Wakuu wa Idara za Mafunzo za Wizara za Sayansi, Utafiti na Teknolojia za Iran na China wamekubaliana juu ya kuanzishwa kituo cha pamoja cha utoaji mafunzo ya kiufundi na kitaalamu na mafunzo ya teknolojia mpya.
-
Kanani: Watoto wa Palestina daima wamekuwa ni jinamizi kwa Wazayuni
Nov 10, 2023 03:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mjibizo kwa shambulio lililofanywa na utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya Hospitali ya Watoto ya Al-Nasr huko Gaza, na kueleza kwamba: "watoto wa Kipalestina daima wamekuwa ni jinamizi kwa Wazayuni."
-
Iran yaiambia G7: Acheni kuunga mkono mauaji ya watoto Gaza
Nov 09, 2023 23:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewakosoa vikali Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Kundi la G7 kwa kutoa taarifa ya pamoja ya kuilaani Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina (Hamas) sambamba na kuunga mkono mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Amir-Abdollahian: Wakati wa kuendelea jinai za Israel huko Gaza unakaribia mwisho
Nov 09, 2023 10:48Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, muda kuendelea jinai za Israel katikak Ukanda wa Gaza unazidi kuyoyoma haraka.
-
Meja Jenerali Salami: Gaza ni kaburi la Marekani na utawala wa Kizayuni
Nov 09, 2023 09:47Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, hii leo Gaza imekuwa uwanja wa kuzikia Marekani na utawala wa Kizayuni, na utawala naoikalii kwa mabavu Quds hauwezi kurejesha nguvu zake zilizopotea.
-
Qalibaf: Mataifa ya Kiislamu yasimamishe mashambulizi ya Wazayuni
Nov 08, 2023 00:03Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amelaani vikali mashambulizi ya kinyama utawala wa Kizayuni huko Gaza na kusisitiza kuwa, mataifa ya Kiislamu yana wajibu wa kusimamisha dhulma na hujuma hizo za kikatili za Wazayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Iran: Vita vya maangamizi ya kizazi vya Israel vimeua, kujeruhi watu 40,000 Gaza
Nov 07, 2023 10:19Afisa wa ngazi ya juu wa haki za binadamu nchini Iran amesema vita na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza yamepelekea watu zaidi ya 40,000 kuuawa na kujeruhi.