Shirikisho la Soka la Iran laitaka FIFA kuipiga marufuku Israel katika michezo
Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limelitaka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kusitisha shughuli zote za soka za utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na utawala huo kutenda jinai huko Gaza.
Katika barua yake kwa FIFA na mashirika ambayo ni wanachama wake, Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limesema: Kutokana na hatua zisizo za kibinadamu na jinai zinazofanywa na utawala haramu wa Israel huko Palestina hususan mauaji ya umati dhidi ya raia katika Ukanda wa Gaza Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) linapaswa kufungia shughuli zote za soka za utawala haramu wa Israel.
Sehemu nyingine ya barua ya Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasema, hatua ya FIFA inaweza kuzuia kuendelea jinai hizo zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina na kutoa msaada wa chakula, maji ya kunywa, huduma za tiba na dawa kwa watu wasio na hatia na raia wa kawaida.

Vilevile, Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeeleza katika taarifa hii kwamba, hatua ya haraka ya FIFA, vyama vya soka na vyama wanachama itakuwa ishara ya hisani na utekelezaji wa hati ya jamii ya soka katika uga majukumu ya binadamu na itakuwa harakati nzuri na ya kudumu katika historia ya soka.