Pars Today
Rais mteule wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian anatazamiwa kula kiapo cha kulitumikia taifa Julai 30 mwaka huu.
Viongozi wa nchi mbalimbali duniani akiwemo Rais wa Afrika Kusini wameendelea kumpongeza Rais mteule wa Iran, Massoud Pezeshkian kwa kuibuka na ushindi katika duru ya 14 ya uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu.
Msemaji wa Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema umoja huo uko tayari kwa ajili ya kupanua wigo wa ushirikiano wa pande mbili na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Stephane Dujarric Msemaji wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa taasisi hiyo ya kimataifa ina hamu ya kushirikiana na Rais mpya wa Iran, Masoud Pezeshkian.
Rais mteule wa Iran amesema serikali yake ijayo itafanya kile iwezalo kuunga mkono vikosi vya muqawama katika eneo la Asia Magharibi, akisisitiza kuwa kuuunga mkono mrengo wa mapambano ni katika sera kuu za Jamhuri ya Kiislamu.
Bahareh Arabi, Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Hali ya Hewa la Iran amesema wataalamu 2 wa Shirika la Hali ya Hewa la Iran wamechaguliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Huduma ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani.
Mohammad Mokhbrr, Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Rais Xi Jinping wa China walikutana na kujadiliana kando ya Mkutano wa 24 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai huko Astana, mji mkuu wa Kazakhstan.
Muda wa kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Iran iliyoanza mapema leo kote nchini, umerefushwa kwa saa mbili, hiyo ikiwa na maana kuwa zoezi hili litaendelea hadi saa mbili usiku kwa saa za hapa nchini.
Vyombo vya habari vya duniani vimeakisi kwa wingi mno duru ya pili ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kisilamu ya Iran kutokana na watu kujitokeza kwa mamilioni katika uchaguzi huo wa leo Ijumaa.
Kaimu Rais wa Iran amesema uhusiano wa kistratajia baina ya Jamhuri ya Kiislamu na Russia umebadilisha mlingano wa nguvu duniani, na kukabiliana na mfumo usio wa kiadilifu na unaoegemea upande mmoja wa Marekani.