Jul 04, 2024 11:31
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza umuhimu wa kushiriki kwa wingi wananchi katika duru ya pili ya uchaguzi wa Rais wa Iran na kusisitiza kuwa, kadiri ushiriki wa wananchi unavyokuwa mkubwa ndivyo serikali pia itakavyoweza kutimiza malengo yake ndani ya nchi na kufuatilia malengo mbalimbali katika kalibu ya mkakati mkuu wa nchi.