Jul 02, 2024 11:53 UTC
  • Mwanadiplomasia wa Iran atahadharisha kuhusu taathira za vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Mkuu wa Baraza la Kistratejia la Uhusiano wa Nje la Iran ametahadharisha kuhusu mashambulizi yanayoweza kuanzishwa na utawala unaotekeleza mauaji ya kimbari wa Israel dhidi ya Lebanon.

Sayyid Kamal Kharrazi ameeleza kuwa eneo la Asia Magharibi litakabiliwa na hatari ya vita vikubwa; na kwamba Tehran na mhimili wa muqawama zitaisaidia na kuiunga mkono Lebanon na harakati ya Hizbullah kwa suhula zote iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utaishambulia nchi hiyo ya Kiarabu. Sayyid Kharrazi amebainisha haya katika mazungumzo na gazeti la Financial Times la nchini Uingereza.   

Kharrazi ameeleza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina lengo la kuanzisha vita katika eneo hili na inataika Marekani iishinikize Israel ili kuzuia kushtadi zaidi mapigano. 

Mkuu wa Baraza la Kistratejia la Uhusiano wa Nje la Iran pia akijibu swali aliloulizwa na Financial Times kwamba je Iran itaiunga mkono harakati ya Hizbullah au la iwapo kutajiri vita vya pande zote, Sayyid Kamal Kharrazi amesema: "Wananchi wote wa Lebabon, nchi za Kiarabu na wanachama wa mhimili wa muqwama zitaiunga mkono Lebanon mkabala wa Israel."

Wakati huo huo vyombo vya habari vya utawala wa Israel vimekiri kuhusu taathira za vipigo vikali vya wanamuqawama wa Kiislamu wa Lebanon huko kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kutangaza kuwa oparesheni za Hizbullah zimegeuka kuwa vita vya kutoa kichapo na kusambaratisha vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika eneo hilo. 

Oparesheni za Hizbullah dhidi ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni 

 

Tags