Wanajeshi 2 wa Israel waangamizwa kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu
Wanajeshi wawili wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliangamizwa jana katika oparesheni iliyotekelezwa na wanamapambano wa kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Shirika la habari la IRNA limetipoti kuwa, kanali ya 12 ya televisheni ya Israel imetangaza kuwa wanajeshi wawili wa utawala huo wameuawa na mmoja kujeruhiwa katika oparesheni ya wanamapambano wa Palestina kwa kutumia silaha baridi katika kituo cha biashara katika kitongoji cha Karmiel, kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel).
Vyombo vya habari vya Israel pia vimetangaza kuwa wanajeshi wa Kizayuni walimpiga risasi aliyetekeleza oparesheni hiyo.
Kuhusiana na suala hilo, harakati ya Jihadul Islami ya Palestina pia imetoa taraifa na kupongeza oparesheni hiyo ya wanamuqawama dhidi ya Wazayuni katika kitongoji cha Karmiel na kusisitiza juu ya chaguo la mapambano dhidi ya maghasibu wa Kizayuni wanaoikalia Quds kwa mabavu.
Taarifa ya Jihadul Islami imeongeza kuwa, oparasheni ya wanamapambano katika kitongoji cha Wazayuni cha Karmiel imethbitisha kuwa mapambano ndio chaguo pekee la watu wa Palestina kwa ajili ya kuwafurisha maghasibu wa Kizayuni katika ardhi za Palestina na kukabiliana na vita vya mauaji ya kimbari na jinai za kinyama za adui.
Katika upande mwingine, Wizara ya Afya ya Gaza jana Jumatano ilitangaza kuwa Wapalestina 37,953 wameuawa shahidi na 87,266 kujeruhiwa hadi sasa tangu utawala wa Israel uanzishe mashambulizi na mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza Oktoba mwaka jana.
Wizara ya Afya ya Gaza imesema kuwa miili kadhaa ya mashahidi bado iko chini ya vifusi na mashirika ya misaada hayana uwezo wa kuipata na kuisafirisha hadi kwenye vituo vya afya kutokana na kuendelea mashambulizi ya utawala wa Kizayuni.