Makamanda wa Israel: Wanajeshi wamechoshwa na vita Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i113668-makamanda_wa_israel_wanajeshi_wamechoshwa_na_vita_ukanda_wa_gaza
Makamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la utawala ghasibu wa Israel wametahadharisha kuwa wanajeshi wa utawala huo wanakabiliwa na uchovu katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Jul 03, 2024 22:56 UTC
  • Makamanda wa Israel: Wanajeshi wamechoshwa na vita Ukanda wa Gaza

Makamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la utawala ghasibu wa Israel wametahadharisha kuwa wanajeshi wa utawala huo wanakabiliwa na uchovu katika Ukanda wa Gaza.

Makamanda wa jeshi la Israel wamesema kuwa wanajeshi wao wamechoshwa na vita huko Gaza huku mashambulizi ya kikatili na mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa Kipalestina wa eneo hilo yaliyoanzishwa na utawala wa Kizayuni Oktoba mwaka jana, yakiendelea kwa karibu miezi tisa sasa. 

Makamanda wa brigedi nne zinazoshiriki vita Ukanda wa Gaza wamemweleza Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kuwa wanajeshi wao wamechoka na vita katika eneo hilo vinavyoendelea kwa miezi tisa sasa. 

Benjamin Netanyahu 

Israel imewauwa shahidi karibu Wapalestina elfu 40 katika Ukanda wa Gaza tangu utawala huo uanzishe mashambulizi na mauaji ya kimbari Oktoba mwaka jana. 

Makamanda wa kijeshi wa Israel wiki hii walikutana na Netanyahu na kusisitiza haja ya kuwazingatia wanajeshi wao wote waliochoka kupigana vita huko Ukanda wa Gaza.