-
Rouhani: Taifa la Iran linajivunia vikosi vyake vya ulinzi
Apr 21, 2021 23:28Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (Artesh) na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ni vikosi vya ulinzi ambavyo daima vimekuwa katika medani. Ameongeza kuwa, taifa la Iran linajivunia jitihada na kujitolea muhanga kwa vikosi hivyo vya ulinzi katika kipindi cha miaka 42 iliyopita.
-
Marekani yakiri kuhusu nguvu ya Iran ya ndege zake zisizo na rubani (droni)
Apr 21, 2021 22:22Jenerali Kenneth McKenzie, Kamanda wa Kamandi Kuu ya askari wa kigaidi wa Marekani CENTCOM, amekiri kwamba nguvu ya droni za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepunguza na kudhoofisha pakubwa uwezo wa anga wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).
-
Iran haitaruhusu mazungumzo ya Vienna kuhusu JCPOA yawe marefu kupita kiasi
Apr 21, 2021 03:02Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema Jamhuri ya Kiislamu haitamruhusu yeyote ayageuze mazungumzo ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yanayofanyika huko Vienna, mji mkuu wa Austria kuwa marefu kupita kiasi na yasiyo na kikomo.
-
Mbunge wa Bunge la Ulaya: Tofauti na US, Iran iliisaidia Iraq kupambana na ISIS
Apr 21, 2021 02:59Mbunge wa kujitegemea wa Bunge la Ulaya (MEP) amesema kuibuka kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) nchini Iraq ni matokeo ya Marekani kuivamia nchi hiyo ya Kiarabu mwaka 2003; na kwamba kinyume na Marekani, Iran iliinyooshea Baghdad mkono wa msaada na uungaji mkono katika vita dhidi ya genge hilo la kitakfiri.
-
Rouhani: Taifa la Zimbabwe litavishinda vikwazo vya Marekani
Apr 18, 2021 22:24Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia ujumbe wa pongezi mwenzake wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa kwa mnasaba wa Siku ya Uhuru wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, iliyoadhimishwa jana Jumapili.
-
Iran: Kurutubisha urani kwa 60% ni jibu kwa njama za maadui
Apr 18, 2021 22:24Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema urutubishaji wa madini ya urani kwa kiwango cha asilimia 60 hapa nchini ni jibu kwa njama na chokochoko za maadui wa taifa hili.
-
Rais Hassan Rouhani asisitiza kupanuliwa ushirikiano wa Iran na Serbia
Apr 18, 2021 07:50Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya udharura wa kupanuliwa ushirikiano kati ya taifa hili na Serbia.
-
Watu 405 waripotiwa kufariki duniani nchini Iran kwa Covid-19
Apr 18, 2021 07:46Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema kuwa, watu 405 wamefariki dunia kwa Covid-19 nchini Iran katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita na kuifanya idadi ya watu walioaga dunia hadi sasa kwa virusi hivyo hapa nchini kufikia 66,732.
-
Urutubishaji wa madini ya urani hadi asilimia 60 nchini Iran na kelele za kisiasa zilizoibuliwa
Apr 18, 2021 06:19Iran kamwe haifuatilii shughuli zisizo za kawaida za nyuklia na wala haina mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia. Huu ni ukweli ambao umethibitishwa mara kadhaa katika ripoti za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).
-
Iran yajibu matamshi ya kuingilia masuala yake ya ndani yaliyotolewa na Arab League na GCC
Apr 16, 2021 22:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameiasa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi (P) GCC badala ya kuungana na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kutoa tuhuma kila mara dhidi ya Iran zielekeze macho yao kwa shughuli za kijeshi za nyuklia na zilizo kinyume na sheria zinazofanywa na utawala huo.