Ismail Haniya: Iran ndiyo roho ya kambi ya muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i73312-ismail_haniya_iran_ndiyo_roho_ya_kambi_ya_muqawama
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo roho na moyo wa mrengo wa muqawama wa Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 09, 2021 03:11 UTC
  • Ismail Haniya: Iran ndiyo roho ya kambi ya muqawama

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo roho na moyo wa mrengo wa muqawama wa Kiislamu.

Ismail Haniya amesema hayo katika mahojiano yaliyorushwa hewani na televisheni moja ya kitaifa ya Iran na kufafanua kuwa, Jamhuri ya Kiislamu kama roho ya kambi ya muqawama, imeufanyia mengi kwa maneno na vitendo mrengo huo.

Ameashiria uchaguzi mkuu uliofanyika hapa nchini miezi michache iliyopita na kueleza kuwa: Uchaguzi wa urais wa hivi karibuni nchini Iran umeichorea dunia taswira ya ustaarabu mpya wa Kiislamu katika eneo.

Haniya ameeleza bayana kuwa, uwepo wa wawakilishi kutoka nchi mbalimbali duniani katika hafla ya kuapishwa Rais wa Iran iliyofanyika siku chache zilizopita, unaashiria uwezo na ushawishi wa Jamhuri ya Kiislamu, miaka 42 baada ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Haniya (kushoto) alipokutana na Rais mpya wa Iran, Sayyid Ibrahim Raisi hapa Tehran majuzi

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas ya Palestina amesema, mkwaruzano na mipasuko kwenye baraza la mawaziri la utawala haramu wa Israel ni ishara ya wazi ya udhaifu wa utawala huo wa Kizayuni.

Ismail Haniya amebainisha kuwa, "baada ya miongo saba ya mapambano, Wapalestina wanaishi vizuri na salama katika ardhi yao, na daima wapo tayari kwa Intifadha muda wowote."